Javascript must be enabled to continue!
Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
View through CrossRef
Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na jinsi ilivyokuwa kabla Wazungu hawajazuru barani Afrika. Mtafiti analinganisha miktadha ya utendaji wa hadithi na anatoa maelezo kuhusu mitindo mbalimbali ya utendaji. Anaeleza jinsi Waafrika walivyosimulia watoto wao hadithi kabla ya Wazungu kuja barani humu. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni: kudhihirisha athari za usasa kwenye masimulizi ya kinathari. Pili, kueleza stadi zilizokuwa zikitumiwa na Waafrika katika usimulizi wa hadithi. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaanza kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Kabla hajafanya hivyo, mtafiti alijitambulisha kwa wahojiwa wake na kuwaambia sababu za utafiti wake. Alifanya hivyo ili kuwaondolea wasiwasi. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usimulizi wa hadithi umefifia sana katika jamii ya Wamasaaba kutokana na usasa. Sababu ambazo zimepelekea usimulizi wa hadithi kufifia jamii hii pia zimeelezwa. Miongoni mwa sababu hizo ni: ulevi ambao hufanya watu kurejea nyumbani wakiwa wamelewa na kushindwa kusimulia watoto wao hadithi. Sababu nyingine ni wazazi kuthamini elimu ya kisasa na kuacha utamaduni wao wa kulea watoto ili baadaye wawe wake na waume wazuri. Wazazi kuhamasisha watoto wao wasome vitabu badala ya kuwasimulia hadithi. Nne, wazazi kuwa na lengo la kuelimisha watoto wao ili baadaye wapate kazi za afisi. Tano, jambo la kuwepo na utandawazi ambalo limepelekea watu kujumuika na kuiga tamaduni za kigeni. Upeo wa utafiti huu ulihusika na mabadiliko kwenye usimulizi wa hadithi na sababu ambazo zimepelekea utamaduni wa kusimulia hadithi kufifia katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Mtafiti alitumia mbinu ya bahati nasibu kuteua sampuli za wahojiwa.
East African Nature and Science Organization
Title: Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Description:
Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda.
Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na jinsi ilivyokuwa kabla Wazungu hawajazuru barani Afrika.
Mtafiti analinganisha miktadha ya utendaji wa hadithi na anatoa maelezo kuhusu mitindo mbalimbali ya utendaji.
Anaeleza jinsi Waafrika walivyosimulia watoto wao hadithi kabla ya Wazungu kuja barani humu.
Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni: kudhihirisha athari za usasa kwenye masimulizi ya kinathari.
Pili, kueleza stadi zilizokuwa zikitumiwa na Waafrika katika usimulizi wa hadithi.
Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani.
Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaanza kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake.
Kabla hajafanya hivyo, mtafiti alijitambulisha kwa wahojiwa wake na kuwaambia sababu za utafiti wake.
Alifanya hivyo ili kuwaondolea wasiwasi.
Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usimulizi wa hadithi umefifia sana katika jamii ya Wamasaaba kutokana na usasa.
Sababu ambazo zimepelekea usimulizi wa hadithi kufifia jamii hii pia zimeelezwa.
Miongoni mwa sababu hizo ni: ulevi ambao hufanya watu kurejea nyumbani wakiwa wamelewa na kushindwa kusimulia watoto wao hadithi.
Sababu nyingine ni wazazi kuthamini elimu ya kisasa na kuacha utamaduni wao wa kulea watoto ili baadaye wawe wake na waume wazuri.
Wazazi kuhamasisha watoto wao wasome vitabu badala ya kuwasimulia hadithi.
Nne, wazazi kuwa na lengo la kuelimisha watoto wao ili baadaye wapate kazi za afisi.
Tano, jambo la kuwepo na utandawazi ambalo limepelekea watu kujumuika na kuiga tamaduni za kigeni.
Upeo wa utafiti huu ulihusika na mabadiliko kwenye usimulizi wa hadithi na sababu ambazo zimepelekea utamaduni wa kusimulia hadithi kufifia katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda.
Mtafiti alitumia mbinu ya bahati nasibu kuteua sampuli za wahojiwa.
Related Results
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...

