Javascript must be enabled to continue!
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
View through CrossRef
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo. Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo. Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka. Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972. Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga. Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini. Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School. Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70. Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi. Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa. Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari. Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.
East African Nature and Science Organization
Title: Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Description:
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen.
Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka kuchunguza nafasi ya vyombo vya habari katika kuhuisha fasihi simulizi kupitia utanzu wa nyimbo.
Tafiti za awali zilichunguza tanzu nyingine kama mazungumzo na maigizo.
Utafiti huu ulidhamiria hususan: Kubainisha vigezo vilivyotumiwa kuteua nyimbo zinazochezwa kwenye kipindi cha Rauka; Kuonyesha maudhui katika nyimbo teule; Kuchunguza mbinu za lugha zilizotumiwa kuwasilisha maudhui za nyimbo zinazoteuliwa na kuchezwa kwenye kipindi cha Rauka.
Utafiti huu ulifanywa kwa kuzingatia muundo wa kimfano unaoeleza kuwa mtafiti huteua eneo au kitu maalum ambacho kitashughulikiwa na kuwezesha kupatikana kwa data za utafiti zilizokusudiwa.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Ajenda iliyoasisiwa na McCombs na Shaw mwaka wa 1972.
Nadharia ya Ajenda ilitumika kuhakiki uteuzi wa nyimbo wa kipindi kinachopeperushwa na runinga.
Uchunguzi ulifanywa katika idhaa ya Citizen kipindi cha Rauka kinachopeperusha nyimbo za dini.
Utafiti uliwahusisha waandaaji wawili wa kipindi cha Rauka cha runinga ya Citizen na watazamaji 68 kutoka eneo la Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu, shule za upili ya wasichana ya Hill School.
Kwa ujumla, utafiti uliwahusisha watu 70.
Watazamaji waliteuliwa kwa kutumia usampulishaji kimaksudi.
Vifaa vifuatavyo vilitumiwa kukusanya data: hojaji kwa watazamaji, usaili kwa waandaaji wa kipindi na mwalimu msimamizi wa masuala ya dini na mkuu wa ushauri na nasaha na kinasa sauti kunasia vipindi vilivyoteuliwa kisha vikachanganuliwa.
Data ifuatayo ilikusanywa: Nyimbo zilizochezwa kwenye kipindi cha Rauka ziliteuliwa kwa kuzingatia mada ya siku, muda uliotengewa kipindi cha Rauka, hadhira, masuala ibuka, kuwepo na nyimbo zinazowavutia watazamaji; Utafiti umebainisha kuwa nyimbo zinazochezwa katika kipindi cha Rauka zina maudhui ya upendo, shukrani, msamaha, uvumilivu, heshima, wema na msaada.
Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kuzingatia nadharia ya Ajenda kwa kubainisha maudhui yaliyomo kisha matokeo yakawasilishwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mfano.
Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mchango kwa tafiti ambazo zimefanywa kuhusu fasihi simulizi na matumizi yake katika vyombo vya habari.
Utafiti huu vilevile utakuwa wa manufaa kwa yeyote atakayefanya utafiti kuhusu fasihi simulizi na vyombo vya habari.
Related Results
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyim...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Uchanganuzi wa Maudhui na Wahusika Kibibliotherapia katika Hadithi Fupi Teule za Kiswahili
Uchanganuzi wa Maudhui na Wahusika Kibibliotherapia katika Hadithi Fupi Teule za Kiswahili
Bibliotherapia ni mbinu muhimu inayoweza kutumiwa kama kipumuo kwa vijana kwa baadhi ya matatizo
yanayowakumba katika kipindi fulani cha maisha yao. Bibliotherapia humsaidia ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizowe...

