Javascript must be enabled to continue!
Uchanganuzi wa Maudhui na Wahusika Kibibliotherapia katika Hadithi Fupi Teule za Kiswahili
View through CrossRef
Bibliotherapia ni mbinu muhimu inayoweza kutumiwa kama kipumuo kwa vijana kwa baadhi ya matatizo
yanayowakumba katika kipindi fulani cha maisha yao. Bibliotherapia humsaidia msomaji kupitia mtagusano
wake na maudhui na wahusika ambao wamepitia hali kama ya yule msomaji. Makala haya yalilenga
kuchanganua maudhui na uhusika ili kubaini sifa za kibibliotherapia katika diwani hizi za hadithi fupi;MayaiWaziri wa Maradhi na hadithi nyingine (2004),Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine(2007),Kiti cha Moyoni na hadithi nyingine (2007)na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016).Mbinu iliyotumiwa kukusanya data hii ni majadiliano katika makundi au kundi lengani. Utafiti huu ulipata matini yake kutoka kwa hadithi fupi teule zinazotumiwa au zinazoweza kutumiwa kama matini ya fasihi ya Kiswahili katika shule za upili. Utafiti huu ulichukua sampuli kutoka kwa shule 7 za Serikali katika eneo la utafiti. Eneo la utafiti ni kaunti ya Nairobi. Sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu zifuatazo; kimakusudi, kinasibu na utabakishaji. Watafitiwa walikuwa walimu 28 pamoja na wanafunzi 112 wa Kidato cha Tatu wa fasihi ya Kiswahili ambao walizisoma hadithi fupi teule na kutathmini sifa za kibibliotherapia.Kazi hii iliongozwa na mihimili ya nadharia ya Mapatano ya Mwitikio wa Msomaji yake Rosenblatt(1995). Mijadala ya kundi lengani ilionyesha kwamba hadithi fupi zinazosomwa darasani ni za kuaminika na maudhui yanaeleweka vizuri .Ufaafu wa maudhui na wahusika kwa mahitaji ya wanafunzi ni muhimu ili faida za kibibliotherapia zipatikane.
Editon Consortium Publishing
Title: Uchanganuzi wa Maudhui na Wahusika Kibibliotherapia katika Hadithi Fupi Teule za Kiswahili
Description:
Bibliotherapia ni mbinu muhimu inayoweza kutumiwa kama kipumuo kwa vijana kwa baadhi ya matatizo
yanayowakumba katika kipindi fulani cha maisha yao.
Bibliotherapia humsaidia msomaji kupitia mtagusano
wake na maudhui na wahusika ambao wamepitia hali kama ya yule msomaji.
Makala haya yalilenga
kuchanganua maudhui na uhusika ili kubaini sifa za kibibliotherapia katika diwani hizi za hadithi fupi;MayaiWaziri wa Maradhi na hadithi nyingine (2004),Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine(2007),Kiti cha Moyoni na hadithi nyingine (2007)na Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (2016).
Mbinu iliyotumiwa kukusanya data hii ni majadiliano katika makundi au kundi lengani.
Utafiti huu ulipata matini yake kutoka kwa hadithi fupi teule zinazotumiwa au zinazoweza kutumiwa kama matini ya fasihi ya Kiswahili katika shule za upili.
Utafiti huu ulichukua sampuli kutoka kwa shule 7 za Serikali katika eneo la utafiti.
Eneo la utafiti ni kaunti ya Nairobi.
Sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu zifuatazo; kimakusudi, kinasibu na utabakishaji.
Watafitiwa walikuwa walimu 28 pamoja na wanafunzi 112 wa Kidato cha Tatu wa fasihi ya Kiswahili ambao walizisoma hadithi fupi teule na kutathmini sifa za kibibliotherapia.
Kazi hii iliongozwa na mihimili ya nadharia ya Mapatano ya Mwitikio wa Msomaji yake Rosenblatt(1995).
Mijadala ya kundi lengani ilionyesha kwamba hadithi fupi zinazosomwa darasani ni za kuaminika na maudhui yanaeleweka vizuri .
Ufaafu wa maudhui na wahusika kwa mahitaji ya wanafunzi ni muhimu ili faida za kibibliotherapia zipatikane.
Related Results
Usawiri wa mandhari kibibliotherapia katika hadithi fupi teule za kiswahili
Usawiri wa mandhari kibibliotherapia katika hadithi fupi teule za kiswahili
Mandhari huwa ni sehemu muhimu katika kazi ya Sanaa. Mtunzi hutumia mandhari kuibua maudhui na sifa za wahusika. Mandhari ni mahali au makazi maalum yaliyojengwa na mtunzi na mnamo...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...