Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000

View through CrossRef
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika. Kila jamii ina ujumi wake. Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi. Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake. Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika. Makala hii imetumia data za maktabani. Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika. Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu. Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika. Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule. Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule. Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili. Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura. Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana. Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo
East African Nature and Science Organization
Title: Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Description:
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni.
Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura.
Ujumi wa kijamii huwa na dhima muhimu katika kazi za kifasihi za jamii husika.
Kila jamii ina ujumi wake.
Ujumi wa Waafrika huitwa ujumi mweusi.
Huu ni ujumi utokanao na utamaduni wa jamii ya Kiafrika pamoja na mazingira yake.
Ujumi huu huweza kutumika kuhakikia kazi za kifasihi za Kiafrika.
Makala hii imetumia data za maktabani.
Jumla ya nyimbo 8 za kuanzia mwaka 1970-2000 zimetumika.
Nyimbo hizo zimeteuliwa kimakusudi, kwa kutumia usampulishaji usonasibu.
Uteuzi huo umefanywa kwa zingatia dhima kuu, na ya kipekee, inayojitokeza zaidi kwenye wimbo husika.
Mbinu zilizotumika kukusanyia data ni; utazamaji makini, udurusu wa matini na mbinu ya kutalii na kukusanya.
Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, na nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data ya utafiti huu.
Matokeo ya utafiti wa makala hii yanabainisha kwamba ujumi mweusi una mchango mkubwa katika unusura wa nyimbo teule.
Unusura huo umebainika kusababishwa na usawiri, kwa mawanda mapana vipengele mbalimbali vya ujumi mweusi kwenye nyimbo teule.
Vipengele hivyo ni; umoja na ushirika, adabu na utii, utu, na matumizi bora ya lugha ya Kiswahili.
Hivyo, walengwa wake huvutika kuzisikiliza kwani hugusa mambo yanayojenga ustawi wa jamii yao, hivyo kuwa na unusura.
Hivyo, wasanii wanashauriwa kuendelea kutunga nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zenye usawiri wa ujumi mweusi kwa mawanda mapana.
Hali hii itasaidia kuendeleza unusura wa nyimbo hizi, kwa ajii ya usatawi wa jamii ya Watanzania na jamii nyinginezo.

Related Results

Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyim...
UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
Imebainika kuwa tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022). Athari zake zimebai...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Kiswahili Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawir...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

Back to Top