Javascript must be enabled to continue!
UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
View through CrossRef
Imebainika kuwa tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022). Athari zake zimebainika katika vipengele kadhaa vya kibunifu (Kasiga, 2021). Pia, misukumo mbalimbali inayowasukuma wasanii kutumia U-Nigeria imebainishwa (Kasiga, 2022). Kimsingi, hali hii inatishia utambulisho wa Kitanzania katika sanaa. Hivyo, makala hii imetoa mapendekezo ya kiuboreshaji dhidi ya U-Nigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania. Mapendekezo yalitolewa yamehusisha kufanyika uwekezaji wa muziki wa asili wa Kitanzania, kufanyika kwa usimamizi maalumu katika vyombo vya habari, kuwepo kwa sheria na kanuni za kulinda uasili wa muziki wa kizazi kipya, na uanizhwaji wa semina, warsha pamoja na madarasa maalumu kwa wasanii. Pia, makala imependekeza kuwepo kwa agenda mahususi ya kitaifa kujenga uzalendo, kumakinikia mitindo ya sanaa za Kitanzania katika utengenezaji wa muziki, kuharakisha upatikanaji wa vazi la taifa, kuanzishwa kwa vipindi vya uchambuzi wa nyimbo, na wasanii kushawishiwa kutumia mandhari ya Kitanzania katika video zao. Vilevile, imependekezwa kuanzishwa kwa matamasha na tuzo za muziki, asasi za elimu kutengeneza mitaala ya biashara, lugha ya Kiswahili, na utamaduni wa Kitanzania, na kuwe na muumano kati ya biashara, utamaduni na teknolojia.
Title: UIBUKAJI WA U-NIGERIA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI TANZANIA: MASUALA MUHIMU YA KUZINGATIA
Description:
Imebainika kuwa tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje hususani wa Kinigeria (Mrikaria, 2007; Kasiga, 2022).
Athari zake zimebainika katika vipengele kadhaa vya kibunifu (Kasiga, 2021).
Pia, misukumo mbalimbali inayowasukuma wasanii kutumia U-Nigeria imebainishwa (Kasiga, 2022).
Kimsingi, hali hii inatishia utambulisho wa Kitanzania katika sanaa.
Hivyo, makala hii imetoa mapendekezo ya kiuboreshaji dhidi ya U-Nigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania.
Mapendekezo yalitolewa yamehusisha kufanyika uwekezaji wa muziki wa asili wa Kitanzania, kufanyika kwa usimamizi maalumu katika vyombo vya habari, kuwepo kwa sheria na kanuni za kulinda uasili wa muziki wa kizazi kipya, na uanizhwaji wa semina, warsha pamoja na madarasa maalumu kwa wasanii.
Pia, makala imependekeza kuwepo kwa agenda mahususi ya kitaifa kujenga uzalendo, kumakinikia mitindo ya sanaa za Kitanzania katika utengenezaji wa muziki, kuharakisha upatikanaji wa vazi la taifa, kuanzishwa kwa vipindi vya uchambuzi wa nyimbo, na wasanii kushawishiwa kutumia mandhari ya Kitanzania katika video zao.
Vilevile, imependekezwa kuanzishwa kwa matamasha na tuzo za muziki, asasi za elimu kutengeneza mitaala ya biashara, lugha ya Kiswahili, na utamaduni wa Kitanzania, na kuwe na muumano kati ya biashara, utamaduni na teknolojia.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Kiswahili
Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawir...
Kiswahili na Uandishi, Uchapishaji na Usomaji Nchini Tanzania
Kiswahili na Uandishi, Uchapishaji na Usomaji Nchini Tanzania
Makala inaangazia fursa zilizopo katika uandishi na uchapishaji kwa Kiswahili nchini Tanzania, na kuhoji kwa nini mwandishi na mchapishaji hafaidiki kikamilifu na fursa hizo. Ukose...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...