Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Kiswahili na Uandishi, Uchapishaji na Usomaji Nchini Tanzania

View through CrossRef
Makala inaangazia fursa zilizopo katika uandishi na uchapishaji kwa Kiswahili nchini Tanzania, na kuhoji kwa nini mwandishi na mchapishaji hafaidiki kikamilifu na fursa hizo. Ukosefu wa tija katika shughuli hizo umesababisha mdororo mkubwa katika tasnia ya uchapishaji ambayo inajumuisha uandishi, utoaji vitabu, usambazaji na usomaji, na kuwalazimisha waandishi kuacha kuandika, kuacha kuchapisha kazi zao, au kujitafutia mbinu mbadala za kutoa na kusambaza kazi zao. Makala inaeleza kuwa kuzorota kwa usomaji nchini Tanzania ni chanzo kikuu, na pia ni matokeo, ya mdororo huo. Inaelezwa kuwa ufumbuzi wa tatizo hili sharti uanzie katika kutambua uhusiano na mwingiliano uliopo kati ya tasnia ya vitabu, sera ya elimu na mitaala ya lugha. Inasisitizwa kuwa msingi wa maendeleo ya tasnia ya uchapishaji katika mfumo wa ubepari tulio nao ni usomaji; bila kuwa na hadhira pevu ya wasomaji haiwezekani kuwa na tasnia hai ya vitabu. Mitaala ya sasa haiweki uzito katika usomaji; haitambui kwamba, ili kuwa na taifa la wasomaji, usomaji sharti uanzie katika ngazi ya chini kabisa katika shule za elimu ya awali na kuendelezwa hadi shule za msingi na sekondari ili hatimaye litengenezwe taifa la watu wenye tabia na utamaduni wa kusoma. Watu hao ndio watakaokuwa wateja (yaani soko) wa mwandishi na mchapishaji, na ndio watakaoibeba tasnia ya vitabu. Ili kukipata kizazi hicho kipya cha wasomaji, mapendekezo yanatolewa kuhusiana na utoaji wa motisha kwa waandishi, uboreshaji wa mitaala, maktaba za shule na za umma, na uwekezaji katika utoaji na ununuzi wa vitabu vya ziada na ridhaa kwa upande wa serikali na asasi binafsi.
University of Dar es Salaam
Title: Kiswahili na Uandishi, Uchapishaji na Usomaji Nchini Tanzania
Description:
Makala inaangazia fursa zilizopo katika uandishi na uchapishaji kwa Kiswahili nchini Tanzania, na kuhoji kwa nini mwandishi na mchapishaji hafaidiki kikamilifu na fursa hizo.
Ukosefu wa tija katika shughuli hizo umesababisha mdororo mkubwa katika tasnia ya uchapishaji ambayo inajumuisha uandishi, utoaji vitabu, usambazaji na usomaji, na kuwalazimisha waandishi kuacha kuandika, kuacha kuchapisha kazi zao, au kujitafutia mbinu mbadala za kutoa na kusambaza kazi zao.
Makala inaeleza kuwa kuzorota kwa usomaji nchini Tanzania ni chanzo kikuu, na pia ni matokeo, ya mdororo huo.
Inaelezwa kuwa ufumbuzi wa tatizo hili sharti uanzie katika kutambua uhusiano na mwingiliano uliopo kati ya tasnia ya vitabu, sera ya elimu na mitaala ya lugha.
Inasisitizwa kuwa msingi wa maendeleo ya tasnia ya uchapishaji katika mfumo wa ubepari tulio nao ni usomaji; bila kuwa na hadhira pevu ya wasomaji haiwezekani kuwa na tasnia hai ya vitabu.
Mitaala ya sasa haiweki uzito katika usomaji; haitambui kwamba, ili kuwa na taifa la wasomaji, usomaji sharti uanzie katika ngazi ya chini kabisa katika shule za elimu ya awali na kuendelezwa hadi shule za msingi na sekondari ili hatimaye litengenezwe taifa la watu wenye tabia na utamaduni wa kusoma.
Watu hao ndio watakaokuwa wateja (yaani soko) wa mwandishi na mchapishaji, na ndio watakaoibeba tasnia ya vitabu.
Ili kukipata kizazi hicho kipya cha wasomaji, mapendekezo yanatolewa kuhusiana na utoaji wa motisha kwa waandishi, uboreshaji wa mitaala, maktaba za shule na za umma, na uwekezaji katika utoaji na ununuzi wa vitabu vya ziada na ridhaa kwa upande wa serikali na asasi binafsi.

Related Results

Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...

Back to Top