Javascript must be enabled to continue!
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
View through CrossRef
Kiswahili
Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964). Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika. Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo. Mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoni. Umma lengwa ulihusisha nyimbo za kizazi kipya na mtandao. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za kulevya na mtandao wa You Tube. Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika utabakisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati iliyosawiriwa. Jumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa. Kazi hii ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo. Matokeo ya kazi hii ni kwamba nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya mihadarati. Makala haya yanapendekeza mitandao mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya mihadarati. Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya. Hatimaye, madhara ya mihadarati pia zitafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga.
English
Drug and substance abuse are among emerging issues with dire effects on the community, with the internet as a contributor. The fight against drug and substance abuse was portrayed through highlighting its effects on hip hop songs online. The paper was guided by the Mass Media Effect Theory of Marshall McLuhan in 1964. This paper adopted descriptive action design. The method of research was content analysis. The data on hip-hop songs on YouTube were observed using the content analysis tool. The target group was hip hop songs, drugs and substances and the internet. Purposive sampling was used to select Kiswahili hip hop songs, drug and substance abuse and YouTube. Stratified sampling classified songs thematically and in groups based on similar drugs. The paper targeted five songs on YouTube. It aimed at getting descriptive data. The data collected was quantitatively analysed and presented descriptively from extracts of songs and content analysis schedules. The study found that hip hop songs highlighted the effects of drug and substance abuse on the addicts, their families and society at large. There is a need for other internet platforms, such as Facebook and X, among others, to be studied on the effects of drug and substance abuse. Secondly, the effects of drug and substance abuse are to be studied on other songs apart from hip hop songs. Lastly, the effects of drugs and substance abuse should be studied on other genres of oral literature such as comedy, film and television programs.
Editon Consortium Publishing
Title: Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Description:
Kiswahili
Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii.
Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawiriwa katika mapambano dhidi ya mihadarati kupitia nyimbo za kizazi kipya mtandaoni.
Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Athari ya Vyombo vya Habari iliyoasisiwa na McLuhan’s (1964).
Muundo wa kithamano mkabala wa kiutendaji ulitumika.
Mbinu ya ukusanyaji data iliyotumika ni uchanganuzi wa yaliyomo.
Mwongozo wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data mtandaoni.
Umma lengwa ulihusisha nyimbo za kizazi kipya na mtandao.
Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika kuchagua nyimbo za kizazi kipya za Kiswahili, suala la dawa za kulevya na mtandao wa You Tube.
Kisha, usampulishaji wa kitabaka ulitumika utabakisha nyimbo kidhima na kwa kurejelea aina tofauti ya mihadarati iliyosawiriwa.
Jumla ya nyimbo tano na mtandao mmoja ulilengwa.
Kazi hii ililenga kupata data ya kimaelezo iliyowasilishwa kwa kutumia maelezo ya kifafanuzi, mijadala, mifano na dondoo.
Matokeo ya kazi hii ni kwamba nyimbo za kizazi kipya ziliangazia athari zake kwa jamii, familia na waraibu wa dawa tofauti za kulevya kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii katika mapambano dhidi ya mihadarati.
Makala haya yanapendekeza mitandao mbalimbali tofauti na ule wa YouTube kutafitiwa kwa kurejelea madhara ya mihadarati.
Pili, uchunguzi wa athari ya uraibu wa mihadarati kwa kurejelea nyimbo nyinginezo mbali na zile za kizazi kipya.
Hatimaye, madhara ya mihadarati pia zitafitiwe katika tanzu nyingine za fasihi pepe kama vile vichekesho, filamu na vipindi vya runinga.
English
Drug and substance abuse are among emerging issues with dire effects on the community, with the internet as a contributor.
The fight against drug and substance abuse was portrayed through highlighting its effects on hip hop songs online.
The paper was guided by the Mass Media Effect Theory of Marshall McLuhan in 1964.
This paper adopted descriptive action design.
The method of research was content analysis.
The data on hip-hop songs on YouTube were observed using the content analysis tool.
The target group was hip hop songs, drugs and substances and the internet.
Purposive sampling was used to select Kiswahili hip hop songs, drug and substance abuse and YouTube.
Stratified sampling classified songs thematically and in groups based on similar drugs.
The paper targeted five songs on YouTube.
It aimed at getting descriptive data.
The data collected was quantitatively analysed and presented descriptively from extracts of songs and content analysis schedules.
The study found that hip hop songs highlighted the effects of drug and substance abuse on the addicts, their families and society at large.
There is a need for other internet platforms, such as Facebook and X, among others, to be studied on the effects of drug and substance abuse.
Secondly, the effects of drug and substance abuse are to be studied on other songs apart from hip hop songs.
Lastly, the effects of drugs and substance abuse should be studied on other genres of oral literature such as comedy, film and television programs.
Related Results
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Maneno katika S. E. D. ambayo Hutumika katika Kiswahili Sanifu
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ –English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchun...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...

