Javascript must be enabled to continue!
Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab
View through CrossRef
Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti. Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi, nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika nyimbo za taarab. Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti zao. Kutokana na upekuzi wa kina wa mtafiti, hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo za taarab. Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotiki. Nadharia hii iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983) na Charles Pierce (1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo. Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo teule za taarab. Data ya kimsingi iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina. Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari kuhusu masuala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine. Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa na waimbaji wa nyimbo teule za taarab
East African Nature and Science Organization
Title: Maudhui ya Ukungwi katika Nyimbo Teule za Taarab
Description:
Nyimbo za taarab zimetafitiwa na wataalam mbalimbali kwa mitazamo tofautitofauti.
Kutokana na uchunguzi wa kina wa mtafiti, inabainika kuwa tafiti za awali kuhusu nyimbo za taarab, zimeegemezwa kwenye uchunguzi wa mafumbo katika taarab, masuala ya itikadi, nafasi ya mwanamke katika nyimbo za taarab usimulizi pamoja na uchanganuzi wa taswira katika nyimbo za taarab.
Swala la jumbe za nyimbo za taarab kufungamana na mambo ya kijamii yakiwemo utamaduni limetajwa tu kijuujuu katika tafiti zao.
Kutokana na upekuzi wa kina wa mtafiti, hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu dhima ya kungwi inavyotekelezwa na baadhi ya nyimbo za taarab.
Utafiti huu ulihusu ubainishaji wa maudhui ya ukungwi katika nyimbo teule za taarab.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Simiotiki.
Nadharia hii iliasisiwa na Ferdinand Dessaussure (1983) na Charles Pierce (1998) na inahusu uhusiano uliopo kati ya kitaja na kitajwa na matumizi ya ishara, picha na msimbo.
Nguzo hii ilisaidia katika kufafanua mbinu za uwasilishaji wa ujumbe katika nyimbo teule za taarab.
Data ya kimsingi iliyoichanganuliwa ilikuwa ya maktabani ambapo mtafiti alipakua nyimbo teule kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kuzichanganua kwa kina.
Matokeo yalionyesha kuwa kungwi ana jukumu la kuwafundisha wanawari kuhusu masuala ya unyumba yakiwemo usafi wa mwili na nyumba, namna ya kumhudumia mume, namna ya kusema na marafiki na jamaa za mume, matumizi ya vifaa vya kiasili kama vile mbuzi, kinu, mchi ufagio miongoni mwa mengine.
Aidha, maudhui haya ya ukungwi yanafundishwa na waimbaji wa nyimbo teule za taarab.
Related Results
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Maudhui katika Nyimbo za Tohara za Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyim...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Kila mtoto huhitaji malezi thabiti katika maisha ili kumkuza katika uadilifu wa siku za baadaye. Utafiti huu ulishughulikia maudhui ya malezi ya watoto kwa kuegemea fasihi ya watot...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Athari ya Uraibu wa Dawa za Kulevya katika Jamii kupitia Nyimbo za Kizazi Kipya Mtandaoni
Kiswahili
Suala la dawa za kulevya ni mojawapo ya masuala ibuka lenye athari kubwa katika jamii huku mtandao ukichangia hali hii. Makala haya yalichunguza madhara yake yalivyosawir...

