Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”

View through CrossRef
Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana. Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana na matini nyingine zilizopo, zilizopita au zijazo. Hata hivyo, Bakhtin haoni kama ushairi una uathiriano na ushairi mwingine sawia kama inavyojitokeza katika riwaya. Baadhi ya wataalamu waliohakiki “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona” wanadai kuwa tenzi hizi zimeathiriana. Makala hii inalenga kudhihirisha uathirianomatini wa kimtindo kati ya “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona” katika ushairi wa Kiswahili. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usemezano ya Bakhtin. Ingawa, kwa mujibu wa nadharia hiyo, riwaya ndio utanzu unaotegemea zaidi uathiriano na matini nyingine kuliko ushairi, makala hii inapanua mawanda yake kwa kuchunguza uathiriano wa kimtindo katika ushairi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwapo kwa uathiriano wa muundo, msamiati, majibizano na tamathali za semi.
Title: Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”
Description:
Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana.
Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana na matini nyingine zilizopo, zilizopita au zijazo.
Hata hivyo, Bakhtin haoni kama ushairi una uathiriano na ushairi mwingine sawia kama inavyojitokeza katika riwaya.
Baadhi ya wataalamu waliohakiki “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona” wanadai kuwa tenzi hizi zimeathiriana.
Makala hii inalenga kudhihirisha uathirianomatini wa kimtindo kati ya “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona” katika ushairi wa Kiswahili.
Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Usemezano ya Bakhtin.
Ingawa, kwa mujibu wa nadharia hiyo, riwaya ndio utanzu unaotegemea zaidi uathiriano na matini nyingine kuliko ushairi, makala hii inapanua mawanda yake kwa kuchunguza uathiriano wa kimtindo katika ushairi.
Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwapo kwa uathiriano wa muundo, msamiati, majibizano na tamathali za semi.

Related Results

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...

Back to Top