Javascript must be enabled to continue!
Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
View through CrossRef
Makala hii inalenga kuchambua na kutathmini sifa za kimuundo katika diwani huru ya Rangi ya Anga. Sifa za kimuundo ni muhimu katika kuudhibiti usomaji wa mashairi teule na kumwelekeza msomaji katika kuuelewa ushairi. Ijapokuwa tafiti nyingi zimefanywa kuhusu muundo katika mashairi, pana haja ya kuchambua sifa za kimuundo katika ushairi huru hasa diwani huru ya Rangi ya Anga. Utafiti huu ulitumia nadharia changamano: nadharia ya uhakiki ya umuundo na nadharia ya uhakiki wa kimtindo. Nadharia ya uhakiki ya umuundo iliasisiwa na Ferdinand De Saussure karne ya ishirini. Mawazo yake yaliendelezwa na Culler (1975) aliyeangazia umuundo katika ushairi. Alisisitiza kwamba ushairi ni ishara zinazojisimamia bila kudhibitiwa na mtunzi na ufasiri wa maana unatokana na namna vipengee vya kimuundo huchagizana kimaana. Kutokana na nadharia hii kutokuwa na urejelezi wa nje, nadharia ya uhakiki wa kimtindo ilitumika kufidia udhaifu huu. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa kimtindo iliyoasisiwa na Coombes (1953) na kuendelezwa na Leech (1969). Mihimili mitatu ilitumika kuuongoza utafiti. Mathalan, viwango vya kimofolojia na kisintaksia ni msingi mkuu wa lugha unaodhibiti matumizi ya lugha, matumizi ya maumbo ya picha huonyesha umilisi wa mtunzi katika kuelezea hisia zake na vipashio mbalimbali vya muundo huingiliana na kujengana. Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimaksudi kuteua diwani huru ya Rangi ya Anga (2014) kutokana na matumizi ya miundo tengemano na wepesi wa mawazo ya mtunzi. Uhakiki wa sifa za kimuundo ulizingatia sampuli ya kimaksudi ya mashairi teule, tasnifu, majarida na tahakiki. Data ya pili ilijumuisha mahojiano na mtunzi Kithaka wa Mberia. Matokeo ya data yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Yalionyesha kuwa sifa za kimuundo ni za kimsingi katika utunzi wa mashairi teule, ujenzi wa wizani na kudhibiti usomaji. Utafiti huu unapendekeza wasomaji wa ushairi huru wazingatie sifa za kimuundo ili kuufasiri ujumbe ipasavyo.
East African Nature and Science Organization
Title: Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
Description:
Makala hii inalenga kuchambua na kutathmini sifa za kimuundo katika diwani huru ya Rangi ya Anga.
Sifa za kimuundo ni muhimu katika kuudhibiti usomaji wa mashairi teule na kumwelekeza msomaji katika kuuelewa ushairi.
Ijapokuwa tafiti nyingi zimefanywa kuhusu muundo katika mashairi, pana haja ya kuchambua sifa za kimuundo katika ushairi huru hasa diwani huru ya Rangi ya Anga.
Utafiti huu ulitumia nadharia changamano: nadharia ya uhakiki ya umuundo na nadharia ya uhakiki wa kimtindo.
Nadharia ya uhakiki ya umuundo iliasisiwa na Ferdinand De Saussure karne ya ishirini.
Mawazo yake yaliendelezwa na Culler (1975) aliyeangazia umuundo katika ushairi.
Alisisitiza kwamba ushairi ni ishara zinazojisimamia bila kudhibitiwa na mtunzi na ufasiri wa maana unatokana na namna vipengee vya kimuundo huchagizana kimaana.
Kutokana na nadharia hii kutokuwa na urejelezi wa nje, nadharia ya uhakiki wa kimtindo ilitumika kufidia udhaifu huu.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa kimtindo iliyoasisiwa na Coombes (1953) na kuendelezwa na Leech (1969).
Mihimili mitatu ilitumika kuuongoza utafiti.
Mathalan, viwango vya kimofolojia na kisintaksia ni msingi mkuu wa lugha unaodhibiti matumizi ya lugha, matumizi ya maumbo ya picha huonyesha umilisi wa mtunzi katika kuelezea hisia zake na vipashio mbalimbali vya muundo huingiliana na kujengana.
Utafiti huu ulitumia sampuli ya kimaksudi kuteua diwani huru ya Rangi ya Anga (2014) kutokana na matumizi ya miundo tengemano na wepesi wa mawazo ya mtunzi.
Uhakiki wa sifa za kimuundo ulizingatia sampuli ya kimaksudi ya mashairi teule, tasnifu, majarida na tahakiki.
Data ya pili ilijumuisha mahojiano na mtunzi Kithaka wa Mberia.
Matokeo ya data yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Yalionyesha kuwa sifa za kimuundo ni za kimsingi katika utunzi wa mashairi teule, ujenzi wa wizani na kudhibiti usomaji.
Utafiti huu unapendekeza wasomaji wa ushairi huru wazingatie sifa za kimuundo ili kuufasiri ujumbe ipasavyo.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
'Akapapa'anga Ara Tangata: Genealogising the (Cook Islands) Māori imaginary
'Akapapa'anga Ara Tangata: Genealogising the (Cook Islands) Māori imaginary
<p><b>For Cook Islands Māori (Māori) peoples, genealogical practices, or what is referred to as ‘akapapa‘anga ara tangata (‘akapapa‘anga), are central to identity-makin...

Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu