Javascript must be enabled to continue!
Uhawilishaji Mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Kiswahili kama Lugha ya Pili : Uchunguzi kifani wajifunzaji Warundi nchini Burundi
View through CrossRef
Kiswahili
Makala hii imechunguza uhawilishaji mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Warundi wanaojifunza lugha hiyo kama lugha ya pili. Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna mkazo unahama kutoka silabi moja hadi nyingine kwenye maneno yaliyodhihirisha uhawilishaji mkazo kwa wajifunzaji. Data zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji wa Kiswahili vyuo vikuu viwili vya serikali nchini Burundi. Sampuli ya utafiti ni wanafunzi 20, 10 kutoka Chuo Kikuu cha Ualimu na 10 kutoka Chuo Kikuu cha Burundi. Sampuli hiyo ya wanafunzi ishirini iliteuliwa kuanzia dawati la kwanza hadi la mwisho huku akiruka dawati moja moja. Alifanya hivyo kwa kila darasa. Baada ya kumaliza kazi hiyo ya kuchagua wanafunzi mtafiti aliomba waliochaguliwa kusimulia hadithi wanazojua mmoja hadi mwingine huku akirekodi masimulizi kwa ajili ya uchambuzi wa baadaye. Ili kufikia lengo la makala hii watafiti walitumia mbinu ya masimulizi ya hadithi. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Mizani ambacho ni kiunzi cha nadharia kilichopendekezwa na Liberman (1977) baadaye kikaendelezwa na Liberman na Prince (1977) na Halle na Vergnaud (1978). Watafiti walitumia pia programu ya ″Praat″ katika kuonesha namna nguvumsikiko ulivyokuwa katika kila kiambajengo. Vilevile, watafiti wametumia matawi katika kuonesha utofauti wa gridi kwenye silabi zinazounda neno. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa Warundi huhamisha mkazo kutoka silabi ya mwisho kasoro moja kwenda katika silabi nyingine tofauti katika maneno teule. Kadhalika, makala hii imependekeza kwa tafiti fuatizi yafuatayo: utafiti mwingine ufanyike vijiji ili kuona kuwa hali kama hiyo ipo, utafiti mwingine uchunguza kiimbo, kidatu, au lafudhi tofauti na mkazo. Isitoshe, utafiti ufanyike ili kuchunguza mbinu zinazotumika kufundishia lugha hiyo ya Kiswahili kama zinafaa au la.
EnglishThis article examines stress transfer in Swahili among Burundian learners studying the language as a second language. The main objective of the article is to investigate how stress shifts from one syllable to another in words that demonstrate stress transfer among learners. Data were collected from Swahili learners at two public universities in Burundi. The research sample consisted of 20 students, 10 from the Teachers’ College University and 10 from the University of Burundi. The sample of 20 students was selected by moving from the first desk to the last, skipping one desk at a time in each classroom. After completing the selection process, the researcher asked the selected students to narrate stories they knew one after another while recording the narratives for later analysis. To achieve the article’s objective, the researchers employed the narrative storytelling method. Data analysis was guided by the Metrical Phonology Theory, a theoretical framework proposed by Liberman (1977) and later developed by Liberman and Prince (1977) and Halle and Vergnaud (1978). The researchers also used the “Praat” software to demonstrate the intensity of stress in each component. Additionally, the researchers utilised metrical grids to illustrate the variation in stress placement across syllables forming a word. The study’s findings indicate that Burundian learners transfer stress from the penultimate syllable to another syllable in selected words. Furthermore, the article recommends the following for future research: conducting another study in rural areas to verify if the same phenomenon exists, investigating intonation, tone, or accents distinct from stress, and examining the teaching methods used for Swahili to determine their effectiveness.
Editon Consortium Publishing
Title: Uhawilishaji Mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Kiswahili kama Lugha ya Pili : Uchunguzi kifani wajifunzaji Warundi nchini Burundi
Description:
Kiswahili
Makala hii imechunguza uhawilishaji mkazo wa Kiswahili kwa wajifunzaji Warundi wanaojifunza lugha hiyo kama lugha ya pili.
Lengo kuu la makala hii ni kuchunguza namna mkazo unahama kutoka silabi moja hadi nyingine kwenye maneno yaliyodhihirisha uhawilishaji mkazo kwa wajifunzaji.
Data zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji wa Kiswahili vyuo vikuu viwili vya serikali nchini Burundi.
Sampuli ya utafiti ni wanafunzi 20, 10 kutoka Chuo Kikuu cha Ualimu na 10 kutoka Chuo Kikuu cha Burundi.
Sampuli hiyo ya wanafunzi ishirini iliteuliwa kuanzia dawati la kwanza hadi la mwisho huku akiruka dawati moja moja.
Alifanya hivyo kwa kila darasa.
Baada ya kumaliza kazi hiyo ya kuchagua wanafunzi mtafiti aliomba waliochaguliwa kusimulia hadithi wanazojua mmoja hadi mwingine huku akirekodi masimulizi kwa ajili ya uchambuzi wa baadaye.
Ili kufikia lengo la makala hii watafiti walitumia mbinu ya masimulizi ya hadithi.
Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Mizani ambacho ni kiunzi cha nadharia kilichopendekezwa na Liberman (1977) baadaye kikaendelezwa na Liberman na Prince (1977) na Halle na Vergnaud (1978).
Watafiti walitumia pia programu ya ″Praat″ katika kuonesha namna nguvumsikiko ulivyokuwa katika kila kiambajengo.
Vilevile, watafiti wametumia matawi katika kuonesha utofauti wa gridi kwenye silabi zinazounda neno.
Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa Warundi huhamisha mkazo kutoka silabi ya mwisho kasoro moja kwenda katika silabi nyingine tofauti katika maneno teule.
Kadhalika, makala hii imependekeza kwa tafiti fuatizi yafuatayo: utafiti mwingine ufanyike vijiji ili kuona kuwa hali kama hiyo ipo, utafiti mwingine uchunguza kiimbo, kidatu, au lafudhi tofauti na mkazo.
Isitoshe, utafiti ufanyike ili kuchunguza mbinu zinazotumika kufundishia lugha hiyo ya Kiswahili kama zinafaa au la.
EnglishThis article examines stress transfer in Swahili among Burundian learners studying the language as a second language.
The main objective of the article is to investigate how stress shifts from one syllable to another in words that demonstrate stress transfer among learners.
Data were collected from Swahili learners at two public universities in Burundi.
The research sample consisted of 20 students, 10 from the Teachers’ College University and 10 from the University of Burundi.
The sample of 20 students was selected by moving from the first desk to the last, skipping one desk at a time in each classroom.
After completing the selection process, the researcher asked the selected students to narrate stories they knew one after another while recording the narratives for later analysis.
To achieve the article’s objective, the researchers employed the narrative storytelling method.
Data analysis was guided by the Metrical Phonology Theory, a theoretical framework proposed by Liberman (1977) and later developed by Liberman and Prince (1977) and Halle and Vergnaud (1978).
The researchers also used the “Praat” software to demonstrate the intensity of stress in each component.
Additionally, the researchers utilised metrical grids to illustrate the variation in stress placement across syllables forming a word.
The study’s findings indicate that Burundian learners transfer stress from the penultimate syllable to another syllable in selected words.
Furthermore, the article recommends the following for future research: conducting another study in rural areas to verify if the same phenomenon exists, investigating intonation, tone, or accents distinct from stress, and examining the teaching methods used for Swahili to determine their effectiveness.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
Uchambuzi wa Miktadha ya Kijamii na Mchango Wake katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili Nchini Burundi
Makala hii inahusu miktadha ya kijamii na mchango wake katika kujifunza Kiswahili kama lugha ya pili nchini Burundi. Muktadha wa kijamii huathiri ujifunzaji wa lugha ya pili kwa ku...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto ka...

