Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Matukio ya Mchakato wa Kujiua katika Riwaya ya Rosa Mistika

View through CrossRef
Makala haya yanabainisha baadhi ya matukio ya mchakato wa kujiua yanayosawiriwa katika riwaya ya Rosa Mistika (1971). Lengo la kubainisha matukio hayo ni kuonesha kwamba kujiua si suala linalotokea ghafla, bali ni mchakato ambao huweza kuchukua muda mrefu kabla ya kitendo chenyewe kufanyika. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO, 2018) na gazeti la Habari Leo la Septemba 11 (2019), kujiua ni janga linalotokea kila siku duniani kote na linawaathiri watu wa mataifa, tamaduni, jinsi, dini, na matabaka yote. Data za uchunguzi huu zilipatikana kwa njia ya usomaji na uchambuzi makini wa riwaya ya Rosa Mistika. Kuteuliwa kwa riwaya hii kulitokana na taarifa za awali alizokuwa nazo mwandishi wa makala haya zinazohusu kujiua kwa mhusika mkuu, Rosa. Kwa msingi huo, riwaya hii iliteuliwa kama kiwakilishi cha riwaya nyingine zenye matukio ya kujiua kwa wahusika wake ili kubaini mchakato wa kujiua kwao. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi. Imebainika kuwa katika hali ya kawaida, kujiua huchukuliwa kama kitendo cha ghafla masikioni mwa watu. Hata hivyo, makala haya yamethibitisha kuwa kitendo hicho huwa hakimtokei mhusika kwa ghafla, bali ni mchakato ambao huambatana na matukio, mitanziko, na miktadha mbalimbali ya kimaisha. Hali hii inatokana na ukweli kwamba maisha ya binadamu ni sawa na kitendawili kigumu ambacho jibu lake si rahisi kulipata. Hivyo, kutokana na hilo, siku zote binadamu huyo huwa katika mchakato wa kutaka kutatua kitendawili hicho kwa sababu maisha kwake ni fumbo.
University of Dar es Salaam
Title: Matukio ya Mchakato wa Kujiua katika Riwaya ya Rosa Mistika
Description:
Makala haya yanabainisha baadhi ya matukio ya mchakato wa kujiua yanayosawiriwa katika riwaya ya Rosa Mistika (1971).
Lengo la kubainisha matukio hayo ni kuonesha kwamba kujiua si suala linalotokea ghafla, bali ni mchakato ambao huweza kuchukua muda mrefu kabla ya kitendo chenyewe kufanyika.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO, 2018) na gazeti la Habari Leo la Septemba 11 (2019), kujiua ni janga linalotokea kila siku duniani kote na linawaathiri watu wa mataifa, tamaduni, jinsi, dini, na matabaka yote.
Data za uchunguzi huu zilipatikana kwa njia ya usomaji na uchambuzi makini wa riwaya ya Rosa Mistika.
Kuteuliwa kwa riwaya hii kulitokana na taarifa za awali alizokuwa nazo mwandishi wa makala haya zinazohusu kujiua kwa mhusika mkuu, Rosa.
Kwa msingi huo, riwaya hii iliteuliwa kama kiwakilishi cha riwaya nyingine zenye matukio ya kujiua kwa wahusika wake ili kubaini mchakato wa kujiua kwao.
Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi.
Imebainika kuwa katika hali ya kawaida, kujiua huchukuliwa kama kitendo cha ghafla masikioni mwa watu.
Hata hivyo, makala haya yamethibitisha kuwa kitendo hicho huwa hakimtokei mhusika kwa ghafla, bali ni mchakato ambao huambatana na matukio, mitanziko, na miktadha mbalimbali ya kimaisha.
Hali hii inatokana na ukweli kwamba maisha ya binadamu ni sawa na kitendawili kigumu ambacho jibu lake si rahisi kulipata.
Hivyo, kutokana na hilo, siku zote binadamu huyo huwa katika mchakato wa kutaka kutatua kitendawili hicho kwa sababu maisha kwake ni fumbo.

Related Results

Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...
Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Utafiti huu ulizitathmini sitiari dhanifu ambazo huibuka katika mchakato ufungamanishwao na hafla za majadiliano ya mahari katika awamu mbalimbali za shughuli hiyo muhimu katika ja...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

Back to Top