Javascript must be enabled to continue!
Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
View through CrossRef
Utafiti huu ulizitathmini sitiari dhanifu ambazo huibuka katika mchakato ufungamanishwao na hafla za majadiliano ya mahari katika awamu mbalimbali za shughuli hiyo muhimu katika jamii ya Agikuyu inayorejelewa kama “Ruracio”. Matumizi ya sitiari katika kujenga majadiliano huwa uti wa mgongo na kwa sababu hiyo wawakilishi wanaoteuliwa na pande mbili za aila husika huhitajiwa kuwa na umilisi mpevu wa lugha husika ili kufaulisha shughuli hiyo. Ikumbukwe kuwa, sitiari zinazotumiwa katika mchakato husika huchangia kujenga ukuruba baina ya koo husika kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya Agikuyu popote pale inapojikuta. Data iliyokusanywa ilirekodiwa kutoka mazungumzo halisi ya hafla husika ambapo mtafiti alivihudhuria vikao vitano tofauti lengo likiwa kuipata data ambayo kwa mujibu wa utafiti ingesemwa kuwa tegemevu. Kama mshiriki, mtafiti alizihudhuria hafla mbili katika gatuzi la Muranga na tatu katika gatuzi la Nakuru anakokaa. Data ilitafsiriwa na kuainishwa kwa mujibu wa maratokezi na hatimaye kuelezewa. Sitiari nyingi zilizojitokeza zilifungamana na vitambulisho vya kijinsia. Aidha, sitiari hizo zikijikita katika matukio tofauti tofauti ya mchakato wote wa sherehe hiyo. Ilibainika kuwa, sitiari husheheni hafla hii kwa kiwango kikubwa zikichangia kuingiliana na kukamilisha awamu tofauti tofauti za mitagusano ya jamii hii ya Agikuyu. Matokeo ya utafiti huu bila shaka yatajenga dafina bora ya wasomi katika uwanja wa fasihi na uchanganuzi lugha
East African Nature and Science Organization
Title: Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Description:
Utafiti huu ulizitathmini sitiari dhanifu ambazo huibuka katika mchakato ufungamanishwao na hafla za majadiliano ya mahari katika awamu mbalimbali za shughuli hiyo muhimu katika jamii ya Agikuyu inayorejelewa kama “Ruracio”.
Matumizi ya sitiari katika kujenga majadiliano huwa uti wa mgongo na kwa sababu hiyo wawakilishi wanaoteuliwa na pande mbili za aila husika huhitajiwa kuwa na umilisi mpevu wa lugha husika ili kufaulisha shughuli hiyo.
Ikumbukwe kuwa, sitiari zinazotumiwa katika mchakato husika huchangia kujenga ukuruba baina ya koo husika kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya Agikuyu popote pale inapojikuta.
Data iliyokusanywa ilirekodiwa kutoka mazungumzo halisi ya hafla husika ambapo mtafiti alivihudhuria vikao vitano tofauti lengo likiwa kuipata data ambayo kwa mujibu wa utafiti ingesemwa kuwa tegemevu.
Kama mshiriki, mtafiti alizihudhuria hafla mbili katika gatuzi la Muranga na tatu katika gatuzi la Nakuru anakokaa.
Data ilitafsiriwa na kuainishwa kwa mujibu wa maratokezi na hatimaye kuelezewa.
Sitiari nyingi zilizojitokeza zilifungamana na vitambulisho vya kijinsia.
Aidha, sitiari hizo zikijikita katika matukio tofauti tofauti ya mchakato wote wa sherehe hiyo.
Ilibainika kuwa, sitiari husheheni hafla hii kwa kiwango kikubwa zikichangia kuingiliana na kukamilisha awamu tofauti tofauti za mitagusano ya jamii hii ya Agikuyu.
Matokeo ya utafiti huu bila shaka yatajenga dafina bora ya wasomi katika uwanja wa fasihi na uchanganuzi lugha.
Related Results
Vigezo vya Hymes vya Mawasiliano: Uchanganuzi wa Matukio Kwenye Hafla ya Mazungumzo ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Vigezo vya Hymes vya Mawasiliano: Uchanganuzi wa Matukio Kwenye Hafla ya Mazungumzo ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Lugha kama asasi inajitokeza bayana kama kiunzi muhimu kinacholipambanua kundi fulani la watu kiutamaduni, kijamii na hata kitaifa. Kwa mujibu wa mantiki hii, lugha hukuzwa na kuen...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...

