Javascript must be enabled to continue!
Vigezo vya Hymes vya Mawasiliano: Uchanganuzi wa Matukio Kwenye Hafla ya Mazungumzo ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
View through CrossRef
Lugha kama asasi inajitokeza bayana kama kiunzi muhimu kinacholipambanua kundi fulani la watu kiutamaduni, kijamii na hata kitaifa. Kwa mujibu wa mantiki hii, lugha hukuzwa na kuendelezwa na jamii. Kwa sababu hiyo, matukio ya usemi, aghalabu hutokea kila mahali binadamu anatagusana na mwenzake. Ili kuielewa jamiilugha yoyote ile, kuchunguza jinsi matukio ya usemi yanavyojitokeza ni suala la msingi, hasa wakati wa mazungumzo kuhusu mahari yanapokitwa kwenye imani, utamaduni, malengo, mitazamo na vionjo vya jamiilugha husika. Kutokana na mwelekeo huu, utafiti huu ulichunguza awamu ambazo matukio ya usemi kwenye majadiliano ya mahari katika jamii ya Agikuyu hupitia. Ifahamike, hili huwa suala telezi mno. Utafiti uliwasilisha mfano mahususi wa tukio la usemi la wazungumzaji asilia kwa kuzingatia kaida za kitamaduni za jamiilugha ya Agikuyu. Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa matukio ya usemi katika majadiliano ya mahari katika jamii ya Agikuyu husawiri mabadiliko bayana ya segmenti za usemi kwa mujibu wa mazungumzo kuhusu mahari yakikitwa kwenye imani, utamaduni, malengo, mitazamo na vionjo vya jamiilugha hii yakinasibishwa na vigezo vya Hymes’ (1974) vya ethnografia ya Mawasiliano, MWALEKIHAMKANYA (SPEAKING). Kwenye majadiliano ya mahari husika, matukio ya usemi yaliyodhihirisha kuwapo kwa segmenti mahususi yalihusisha Makaribisho ya kujenga mlahaka, Mazungumzo kuhusu mahari ya posa komavu, Urazinishaji wa kumbukumbu, Kuafiki shabaha ya ujio, Kutakabaliwa kwa ombi, Kuambikwa tambiko na mwisho Kuhitimisha hafla
East African Nature and Science Organization
Title: Vigezo vya Hymes vya Mawasiliano: Uchanganuzi wa Matukio Kwenye Hafla ya Mazungumzo ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Description:
Lugha kama asasi inajitokeza bayana kama kiunzi muhimu kinacholipambanua kundi fulani la watu kiutamaduni, kijamii na hata kitaifa.
Kwa mujibu wa mantiki hii, lugha hukuzwa na kuendelezwa na jamii.
Kwa sababu hiyo, matukio ya usemi, aghalabu hutokea kila mahali binadamu anatagusana na mwenzake.
Ili kuielewa jamiilugha yoyote ile, kuchunguza jinsi matukio ya usemi yanavyojitokeza ni suala la msingi, hasa wakati wa mazungumzo kuhusu mahari yanapokitwa kwenye imani, utamaduni, malengo, mitazamo na vionjo vya jamiilugha husika.
Kutokana na mwelekeo huu, utafiti huu ulichunguza awamu ambazo matukio ya usemi kwenye majadiliano ya mahari katika jamii ya Agikuyu hupitia.
Ifahamike, hili huwa suala telezi mno.
Utafiti uliwasilisha mfano mahususi wa tukio la usemi la wazungumzaji asilia kwa kuzingatia kaida za kitamaduni za jamiilugha ya Agikuyu.
Matokeo ya utafiti huu yalidhihirisha kuwa matukio ya usemi katika majadiliano ya mahari katika jamii ya Agikuyu husawiri mabadiliko bayana ya segmenti za usemi kwa mujibu wa mazungumzo kuhusu mahari yakikitwa kwenye imani, utamaduni, malengo, mitazamo na vionjo vya jamiilugha hii yakinasibishwa na vigezo vya Hymes’ (1974) vya ethnografia ya Mawasiliano, MWALEKIHAMKANYA (SPEAKING).
Kwenye majadiliano ya mahari husika, matukio ya usemi yaliyodhihirisha kuwapo kwa segmenti mahususi yalihusisha Makaribisho ya kujenga mlahaka, Mazungumzo kuhusu mahari ya posa komavu, Urazinishaji wa kumbukumbu, Kuafiki shabaha ya ujio, Kutakabaliwa kwa ombi, Kuambikwa tambiko na mwisho Kuhitimisha hafla.
Related Results
Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Sitiari Dhanifu Katika Mazungumzo ya Hafla ya Mahari Katika Jamii ya Agikuyu
Utafiti huu ulizitathmini sitiari dhanifu ambazo huibuka katika mchakato ufungamanishwao na hafla za majadiliano ya mahari katika awamu mbalimbali za shughuli hiyo muhimu katika ja...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Makala haya yamejikita katika kuchunguza vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Makala haya yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

