Javascript must be enabled to continue!
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
View through CrossRef
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu haukuweka wazi udhihirikaji na matumizi ya mikakati ya upole katika muktadha wa ibada ya mazishi katika lugha ya Kikabrasi na umuhimu wake kwenye mawasiliano. Makala haya yanachunguza udhihirikaji, matumizi, sababu, na umuhimu wa mikakati hii ya upole kwenye hafla za mazishi. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Brown na Levinson (1987). Sampuli ilichaguliwa kimakusudi kutoka hafla kumi na tano za ibada ya mazishi katika kitongoji cha Namanja, eneo bunge la Malava, Kakamega, kwa kuzingatia lugha ya Kikabrasi ikilinganishwa na Kiswahili. Usemi wa wanenaji wa hirimu zote, bila ubaguzi wa jinsia, ulirekodiwa kwa idhini ya utawala wa kijiji na kuwekwa katika kategoria za mikakati ya upole kama ilivyopendekezwa na Brown na Levinson. Matokeo yanaonyesha wazungumzaji hutumia mikakati ya upole, hasa mkakati hasi na mkakati nje ya rekodi, kwa sababu za kunasa hisia za wasikilizaji na kuhifadhi sitara zao, hasa waliofiwa, bila kudhuru sitara zao. Utafiti huu utawezesha wasikilizaji na waombolezaji kupata marifa na ustadi katika kuwahutubia watu wa tabaka mbalimbali katika jamii changamano, na kuongeza data kwa uga wa isimu. Unapendekeza uchunguzi zaidi wa changamoto za mikakati ya upole katika mawasiliano, hasa katika sherehe ya kumbukumbu ya mashujaa na Jukwaa la Facebook.English
The concept of politeness has been widely studied in the field of communication. For instance, the study of politeness in the transport sector among the passengers and the service providers in the Kamba speaking language. However, little attention has been given to the role of politeness strategies in funeral services. This study seeks to address this gap by investigating how politeness strategies are employed in funeral service communication among Kabrasi speakers, guided by Brown and Levinson’s (1987) politeness theory. The sample was purposively drawn from fifteen funeral ceremonies in Namanja Sublocation, Malava Constituency, Kakamega County, with a focus on Kabrasi language use in comparison to Swahili. Speech from participants of all ages and both genders was recorded with the approval of village administration and analysed according to Brown and Levinson’s typology of politeness strategies. Findings indicate that speakers predominantly employ negative and off-record strategies for the purpose of attracting mourners’ attention and protecting their positive image both self and the listeners. Also, speakers use positive and negative politeness strategies more than other politeness strategies for the purpose of condoling and giving message of hope to the bereaved without interfering with their positive image. The study provides insights for mourners and community members on effective communication across diverse social groups in complex communities. It also contributes valuable data to the field of linguistics. The study recommends further research on the challenges of applying politeness strategies in other communicative contexts, such as Mashujaa public holiday and online platforms like Facebook.Keywords: Face, Kabrasi, politeness strategies, widows
Title: Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Description:
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba.
Hata hivyo, utafiti huu haukuweka wazi udhihirikaji na matumizi ya mikakati ya upole katika muktadha wa ibada ya mazishi katika lugha ya Kikabrasi na umuhimu wake kwenye mawasiliano.
Makala haya yanachunguza udhihirikaji, matumizi, sababu, na umuhimu wa mikakati hii ya upole kwenye hafla za mazishi.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Brown na Levinson (1987).
Sampuli ilichaguliwa kimakusudi kutoka hafla kumi na tano za ibada ya mazishi katika kitongoji cha Namanja, eneo bunge la Malava, Kakamega, kwa kuzingatia lugha ya Kikabrasi ikilinganishwa na Kiswahili.
Usemi wa wanenaji wa hirimu zote, bila ubaguzi wa jinsia, ulirekodiwa kwa idhini ya utawala wa kijiji na kuwekwa katika kategoria za mikakati ya upole kama ilivyopendekezwa na Brown na Levinson.
Matokeo yanaonyesha wazungumzaji hutumia mikakati ya upole, hasa mkakati hasi na mkakati nje ya rekodi, kwa sababu za kunasa hisia za wasikilizaji na kuhifadhi sitara zao, hasa waliofiwa, bila kudhuru sitara zao.
Utafiti huu utawezesha wasikilizaji na waombolezaji kupata marifa na ustadi katika kuwahutubia watu wa tabaka mbalimbali katika jamii changamano, na kuongeza data kwa uga wa isimu.
Unapendekeza uchunguzi zaidi wa changamoto za mikakati ya upole katika mawasiliano, hasa katika sherehe ya kumbukumbu ya mashujaa na Jukwaa la Facebook.
English
The concept of politeness has been widely studied in the field of communication.
For instance, the study of politeness in the transport sector among the passengers and the service providers in the Kamba speaking language.
However, little attention has been given to the role of politeness strategies in funeral services.
This study seeks to address this gap by investigating how politeness strategies are employed in funeral service communication among Kabrasi speakers, guided by Brown and Levinson’s (1987) politeness theory.
The sample was purposively drawn from fifteen funeral ceremonies in Namanja Sublocation, Malava Constituency, Kakamega County, with a focus on Kabrasi language use in comparison to Swahili.
Speech from participants of all ages and both genders was recorded with the approval of village administration and analysed according to Brown and Levinson’s typology of politeness strategies.
Findings indicate that speakers predominantly employ negative and off-record strategies for the purpose of attracting mourners’ attention and protecting their positive image both self and the listeners.
Also, speakers use positive and negative politeness strategies more than other politeness strategies for the purpose of condoling and giving message of hope to the bereaved without interfering with their positive image.
The study provides insights for mourners and community members on effective communication across diverse social groups in complex communities.
It also contributes valuable data to the field of linguistics.
The study recommends further research on the challenges of applying politeness strategies in other communicative contexts, such as Mashujaa public holiday and online platforms like Facebook.
Keywords: Face, Kabrasi, politeness strategies, widows.
Related Results
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo. Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikis...
Upole katika Manifesto ya Kenya Kwanza
Upole katika Manifesto ya Kenya Kwanza
Upole ni suala ambalo limeshughulikiwa na wanazuoni mbalimbali katika tamthilia, vipindi vya runinga, mawasiliano ya bodaboda na abiria na mazungumzo ya redioni. Makala hii inadham...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda
Mnyambuliko wa Vitenzi Katika Lugha za Kiafrika: Mfano katika Lugha ya Kimasaaba Nchini Uganda
Katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi vitenzi vya lugha za Kiafrika vinavyonyambuliwa na kuleta maana tofauti tofauti. Anafanya hivyo kwa kurejelea Kimasaaba ambayo ni lugha in...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...

