Javascript must be enabled to continue!
Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
View through CrossRef
Utafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya na kuripotiwa na wanahabari. Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kwamba Serikali ya Kenya na raia wake wameendelea kushuhudia mashambulizi mengi ya ugaidi ambayo yamesababisha kuzuke diskosi ya ugaidi iliyojikita katika ubishi wa kundi la ugaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Ili kupata data ya uchanganuzi, utafiti huu ulihusu uteuzi wa diskosi ya kigaidi kupitia mashambulizi mawili makuu yaliyofanyika nchini Kenya katika duka la kibiashara la West Gate Mall mjini Nairobi na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa mwezi wa Aprili, 2015. Kikundi lengwa kiliteuliwa kutokana na magazeti ya Daily Nation na The Standard yaliyohusu kipindi hicho cha kihistoria. Gazeti la NewYork Times liliteuliwa kutokana na upana wa mkabala wake wa mtazamo wa kimataifa. Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 zikateuliwa za mwanzoni mwa kipindi cha miezi miwili kabla na baada ya mwaka 2013-2015. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia msingi wa Diskosi Mkabala wa Historia ya Wodak iliyotumiwa kuchanganulia mkakati wa lugha katika vitengo vya unominishaji, urejelezi, ubishi, mkabala, uzidishaji na ufifizaji. Uchanganuzi wa mikakati ya lugha ulihusu matumizi ya kijazanda, semi, virai, vishazi na sentensi. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kulikuwako na tofauti za kimkabala zilizozua diskosi ya ubishi kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya. Tofauti hizi zilibainishwa kupitia mikakati ya lugha na itikadi kutokana na mashambulizi ya ugaidi yaliyotekelezwa nchini Kenya
East African Nature and Science Organization
Title: Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
Description:
Utafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Kenya na kuripotiwa na wanahabari.
Sababu kuu ya kuteua kipindi hiki ni kwamba Serikali ya Kenya na raia wake wameendelea kushuhudia mashambulizi mengi ya ugaidi ambayo yamesababisha kuzuke diskosi ya ugaidi iliyojikita katika ubishi wa kundi la ugaidi dhidi ya serikali ya Kenya.
Ili kupata data ya uchanganuzi, utafiti huu ulihusu uteuzi wa diskosi ya kigaidi kupitia mashambulizi mawili makuu yaliyofanyika nchini Kenya katika duka la kibiashara la West Gate Mall mjini Nairobi na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa mwezi wa Aprili, 2015.
Kikundi lengwa kiliteuliwa kutokana na magazeti ya Daily Nation na The Standard yaliyohusu kipindi hicho cha kihistoria.
Gazeti la NewYork Times liliteuliwa kutokana na upana wa mkabala wake wa mtazamo wa kimataifa.
Jumla ya magazeti 145 yalikusanywa na nakala 102 zikateuliwa za mwanzoni mwa kipindi cha miezi miwili kabla na baada ya mwaka 2013-2015.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia msingi wa Diskosi Mkabala wa Historia ya Wodak iliyotumiwa kuchanganulia mkakati wa lugha katika vitengo vya unominishaji, urejelezi, ubishi, mkabala, uzidishaji na ufifizaji.
Uchanganuzi wa mikakati ya lugha ulihusu matumizi ya kijazanda, semi, virai, vishazi na sentensi.
Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa kulikuwako na tofauti za kimkabala zilizozua diskosi ya ubishi kati ya kundi la kigaidi dhidi ya serikali ya Kenya.
Tofauti hizi zilibainishwa kupitia mikakati ya lugha na itikadi kutokana na mashambulizi ya ugaidi yaliyotekelezwa nchini Kenya.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Diskosi za kisiasa hufanya kazi kubwa katika kujenga na kuidhinisha utambulisho wa mwanasiasa, utambulisho wa kikundi chake na uanachama wake. Kupitia lugha, wanasiasa utambulisho ...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...

