Javascript must be enabled to continue!
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
View through CrossRef
Diskosi za kisiasa hufanya kazi kubwa katika kujenga na kuidhinisha utambulisho wa mwanasiasa, utambulisho wa kikundi chake na uanachama wake. Kupitia lugha, wanasiasa utambulisho wa mwanasiasa na ushirika wao kwa kikundi unaweza kugunduliwa kupitia upeaji wa kiutambulisho. Peo ya utambulisho hukuza imani na ukubalifu wa mzungumzaji kwa wasikilizaji wake. Upeaji wa utambulisho, hutegemea uteuzi na utumiaji wa leksia maalumu. Utafiti huu umechunguza upeaji wa kiutambulisho katika diskosi za wabunge wanawake kutoka Bunge la Taifa nchini Kenya. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza leksia zilizotumika katika upeaji wa utambulisho kwenye diskosi za wabunge wanawake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Peo na mtazamo wa Uchanganuzi Hakiki-Makinifu wa Usemi. Nadharia hizi zilitumika kutathmini namna leksia zilizotumika kujenga utambulisho wa jinsia kuhusiana na mamlaka. Chanzo cha data katika utafiti huu; ni video kutoka mtandao wa YouTube ambazo zilikuwa na hotuba zilizowasilishwa kwa umma na wabunge wanawake 169, waliochaguliwa na wananchi katika bunge la 11, 12 na 13 la taifa la Kenya, zilihifadhiwa. Wasailiwa hao ni wanawake 111 wanaowakilisha kaunti pamoja na wanawake 58 waliochaguliwa kuwakilisha maeneobunge mbalimbali katika Bunge la Taifa. Mbinu ya utafiti iliyotumika kukusanywa data ilikuwa utazamaji na usikilizaji wa sauti ninga kutoka kwa mtandao ya YouTube. Utafiti huu umebaini kuwa, matumizi ya kiisimu ya leksia kwenye diskosi za wabunge wanawake hujenga utambulisho kuhusiana na mamlaka, kuambatana mamahitaji ya kibinafsi na kikundi. Leksia katika diskosi za wabunge wanawake, zilitambulisha wanawake katika kiwango cha kibinafsi, kieneo na kimakundi. Kwa hivyo, upeaji wa utambulisho ulidhihirisha migao wa kibinafsi, kimaeneo, kimahusiano, kiutendaji na kimakundi katika ujenzi wa utambulisho wa wanawake.
East African Nature and Science Organization
Title: Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Description:
Diskosi za kisiasa hufanya kazi kubwa katika kujenga na kuidhinisha utambulisho wa mwanasiasa, utambulisho wa kikundi chake na uanachama wake.
Kupitia lugha, wanasiasa utambulisho wa mwanasiasa na ushirika wao kwa kikundi unaweza kugunduliwa kupitia upeaji wa kiutambulisho.
Peo ya utambulisho hukuza imani na ukubalifu wa mzungumzaji kwa wasikilizaji wake.
Upeaji wa utambulisho, hutegemea uteuzi na utumiaji wa leksia maalumu.
Utafiti huu umechunguza upeaji wa kiutambulisho katika diskosi za wabunge wanawake kutoka Bunge la Taifa nchini Kenya.
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza leksia zilizotumika katika upeaji wa utambulisho kwenye diskosi za wabunge wanawake.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Peo na mtazamo wa Uchanganuzi Hakiki-Makinifu wa Usemi.
Nadharia hizi zilitumika kutathmini namna leksia zilizotumika kujenga utambulisho wa jinsia kuhusiana na mamlaka.
Chanzo cha data katika utafiti huu; ni video kutoka mtandao wa YouTube ambazo zilikuwa na hotuba zilizowasilishwa kwa umma na wabunge wanawake 169, waliochaguliwa na wananchi katika bunge la 11, 12 na 13 la taifa la Kenya, zilihifadhiwa.
Wasailiwa hao ni wanawake 111 wanaowakilisha kaunti pamoja na wanawake 58 waliochaguliwa kuwakilisha maeneobunge mbalimbali katika Bunge la Taifa.
Mbinu ya utafiti iliyotumika kukusanywa data ilikuwa utazamaji na usikilizaji wa sauti ninga kutoka kwa mtandao ya YouTube.
Utafiti huu umebaini kuwa, matumizi ya kiisimu ya leksia kwenye diskosi za wabunge wanawake hujenga utambulisho kuhusiana na mamlaka, kuambatana mamahitaji ya kibinafsi na kikundi.
Leksia katika diskosi za wabunge wanawake, zilitambulisha wanawake katika kiwango cha kibinafsi, kieneo na kimakundi.
Kwa hivyo, upeaji wa utambulisho ulidhihirisha migao wa kibinafsi, kimaeneo, kimahusiano, kiutendaji na kimakundi katika ujenzi wa utambulisho wa wanawake.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
Swahili
Makala hii inabainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Suala la urejelezi limechunguzwa na wasomi weng...
Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
Uchanganuzi wa Mikakati ya Lugha katika Diskosi ya Kigaidi katika Magazeti ya Kenya na ya Kimataifa
Utafiti huu ulinuiwa kuchanganulia mikakati ya lugha katika diskosi ya kigaidi kama ilivyotumiwa katika mashambulizi ya kigaidi kati ya kundi la Al-Shabaab dhidi ya serikali ya Ken...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu
na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi A...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Makala haya yamejikita katika kuchunguza vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Makala haya yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali...

