Javascript must be enabled to continue!
Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
View through CrossRef
Swahili
Makala hii inabainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Suala la urejelezi limechunguzwa na wasomi wengi. Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanywa kwa kina kuhusu aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu iliyoendelezwa na Halliday (1985, 1994, 1999), Halliday na Matthiessen (2004) na Matthiessen (2013) kwa kuangazia mtazamo wa Halliday na Hasan (1976). Aidha, Nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Wilson (2003) na Wilson na Sperber (2002) ilitumika kama nadharia changizi katika kufafanua jinsi wasomaji wanavyofikia maana tambuzi katika matini. Mbinu ya makala hii ni ya kimaelezo. Sampuli ya utafiti ilikuwa ya kimakusudi, ambapo nakala 30 za Habari za Kaunti zilizo na aina mbalimbali za urejelezi zilichaguliwa. Data iliyotumika katika makala hii ilikusanywa kutoka gazeti la Taifa Leo kati ya mwezi wa Juni na Julai 2020 kwa ajili ya tasnifu ya uzamili iliyoshughulikia suala la Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa ili kubainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zilivyotumika kuleta mshikamano katika matini. Matokeo yameonyesha kuwa aina mbalimbali za urejelezi zimetumika kuleta mshikamano katika matini. Makala hii inaonyesha kuwa urejelezi wa kiendofora, urejelezi nafsi, urejelezi wa kuashiria na urejelezi wa kulinganisha umetumika katika Habari za Kaunti ili kuleta mshikamano katika matini. Data ya makala hii imewasilishwa kwa kutumia maelezo ili kuonyesha jinsi aina mbalimbali za urejelezi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Utafiti huu utawafaa wasomaji wa gazeti katika kutambua na kufasiri aina mbalimbali za urejelezi kwa njia inayofaa ili kupata habari iliyokusudiwa na mwandishi.English
Title: Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
Description:
Swahili
Makala hii inabainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini.
Suala la urejelezi limechunguzwa na wasomi wengi.
Hata hivyo, hakuna utafiti ambao umefanywa kwa kina kuhusu aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo.
Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Sarufi Amilifu iliyoendelezwa na Halliday (1985, 1994, 1999), Halliday na Matthiessen (2004) na Matthiessen (2013) kwa kuangazia mtazamo wa Halliday na Hasan (1976).
Aidha, Nadharia ya Uhusiano iliyoasisiwa na Wilson (2003) na Wilson na Sperber (2002) ilitumika kama nadharia changizi katika kufafanua jinsi wasomaji wanavyofikia maana tambuzi katika matini.
Mbinu ya makala hii ni ya kimaelezo.
Sampuli ya utafiti ilikuwa ya kimakusudi, ambapo nakala 30 za Habari za Kaunti zilizo na aina mbalimbali za urejelezi zilichaguliwa.
Data iliyotumika katika makala hii ilikusanywa kutoka gazeti la Taifa Leo kati ya mwezi wa Juni na Julai 2020 kwa ajili ya tasnifu ya uzamili iliyoshughulikia suala la Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki.
Data iliyokusanywa ilichanganuliwa ili kubainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zilivyotumika kuleta mshikamano katika matini.
Matokeo yameonyesha kuwa aina mbalimbali za urejelezi zimetumika kuleta mshikamano katika matini.
Makala hii inaonyesha kuwa urejelezi wa kiendofora, urejelezi nafsi, urejelezi wa kuashiria na urejelezi wa kulinganisha umetumika katika Habari za Kaunti ili kuleta mshikamano katika matini.
Data ya makala hii imewasilishwa kwa kutumia maelezo ili kuonyesha jinsi aina mbalimbali za urejelezi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini.
Utafiti huu utawafaa wasomaji wa gazeti katika kutambua na kufasiri aina mbalimbali za urejelezi kwa njia inayofaa ili kupata habari iliyokusudiwa na mwandishi.
English
.
Related Results
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu
na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi A...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Diskosi za kisiasa hufanya kazi kubwa katika kujenga na kuidhinisha utambulisho wa mwanasiasa, utambulisho wa kikundi chake na uanachama wake. Kupitia lugha, wanasiasa utambulisho ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...

