Javascript must be enabled to continue!
Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
View through CrossRef
Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu
na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi Agosti 31, 2019. Utafiti uliongozwa na nadharia ya kimtindo ya Leech na Short (2007) ili kuafikia lengo letu. Mihimili mitatu ya nadharia hii ilitumiwa ili kufanikisha lengo la mtafiti, nayo ni: Fasihi ni muundo wa
lugha na kwa hivyo lazima matumizi ya lugha yazingatiwe, uhakiki wa kifasihi haupaswi kupuuza matumizi ya vipengele vya isimu lugha ikiwemo. Data iliyotumiwa katika utafiti ilikusanywa maktabani na mitandaoni kupitia usomaji wa tasnifu, vitabu, majarida
na magazeti. Uteuzi sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua mashairi yaliyosheheni upya katika mikondo.Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia kwa maelezo.Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba,mashairi ya ushairi wenu na sokomoko yanasheheni mikondo mipya ya utunzi ikiwemo: Matumizi ya Sheng’,usimulizi na kuwepo kwa mianzo ya kifomula. Mashairi yaliyotumika yalitolewa katika kumbi za Sokomoko na Ushairi Wenu ambazo ni kumbi zinazochapisha mashairi ya watunzi mbalimbali katika gazeti la Taifa Leo.Matokeo ya utafiti yalionesha namna mikondo mipya ya utunzi inaendelea kuibuliwa na watunzi wa mashairi kila uchao. Mashairi yaliyotumika hapa hata hivyo, ni yale ya kiarudhi pekee kwani ndiyo yachapishwayo katika gazeti la Taifa Leo.Makala haya yatakuwa ya manufaa kwa walimu wa Kiswahili, wanafunzi na watafiti wengine wanaotafitia suala la upya katika utunzi wa mashairi.
Editon Consortium Publishing
Title: Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Description:
Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu
na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi Agosti 31, 2019.
Utafiti uliongozwa na nadharia ya kimtindo ya Leech na Short (2007) ili kuafikia lengo letu.
Mihimili mitatu ya nadharia hii ilitumiwa ili kufanikisha lengo la mtafiti, nayo ni: Fasihi ni muundo wa
lugha na kwa hivyo lazima matumizi ya lugha yazingatiwe, uhakiki wa kifasihi haupaswi kupuuza matumizi ya vipengele vya isimu lugha ikiwemo.
Data iliyotumiwa katika utafiti ilikusanywa maktabani na mitandaoni kupitia usomaji wa tasnifu, vitabu, majarida
na magazeti.
Uteuzi sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua mashairi yaliyosheheni upya katika mikondo.
Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia kwa maelezo.
Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba,mashairi ya ushairi wenu na sokomoko yanasheheni mikondo mipya ya utunzi ikiwemo: Matumizi ya Sheng’,usimulizi na kuwepo kwa mianzo ya kifomula.
Mashairi yaliyotumika yalitolewa katika kumbi za Sokomoko na Ushairi Wenu ambazo ni kumbi zinazochapisha mashairi ya watunzi mbalimbali katika gazeti la Taifa Leo.
Matokeo ya utafiti yalionesha namna mikondo mipya ya utunzi inaendelea kuibuliwa na watunzi wa mashairi kila uchao.
Mashairi yaliyotumika hapa hata hivyo, ni yale ya kiarudhi pekee kwani ndiyo yachapishwayo katika gazeti la Taifa Leo.
Makala haya yatakuwa ya manufaa kwa walimu wa Kiswahili, wanafunzi na watafiti wengine wanaotafitia suala la upya katika utunzi wa mashairi.
Related Results
Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
Aina za Urejelezi katika Gazeti la Taifa Leo: Mtazamo wa Kipragmatiki
Swahili
Makala hii inabainisha aina za urejelezi katika gazeti la Taifa Leo na jinsi zinavyochangia kuleta mshikamano katika matini. Suala la urejelezi limechunguzwa na wasomi weng...
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.
Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari vya siasa kwenye gazeti la Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charl...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Leksia katika Diskosi za Wabunge Wanawake kutoka Bunge la Taifa Zinazojenga Utambulisho Kuhusiana na Mamlaka
Diskosi za kisiasa hufanya kazi kubwa katika kujenga na kuidhinisha utambulisho wa mwanasiasa, utambulisho wa kikundi chake na uanachama wake. Kupitia lugha, wanasiasa utambulisho ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
Makala hii inalenga kuchambua na kutathmini sifa za kimuundo katika diwani huru ya Rangi ya Anga. Sifa za kimuundo ni muhimu katika kuudhibiti usomaji wa mashairi teule na kumwelek...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo
Makala haya yamejikita katika kuchunguza vigezo vya utoaji majina ya asili ya watu katika jamiilugha ya Wagogo. Makala haya yameongozwa na swali moja katika kuandaliwa kwake. Swali...

