Javascript must be enabled to continue!
Lugha, Mawasiliano na Mizozo: Mikakati ya Mawasiliano katika Kesi za Mizozo kwenye Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu
View through CrossRef
Makala hii inalenga kuchunguza mikakati ya mawasiliano inayotumika katika kesi za migogoro ya umiliki wa ardhi katika Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Ujihusishaji iliyoasisiwa na Giles (1973) na kuendelezwa na Giles et al. (1991). Nadharia hii inaeleza kuwa washiriki katika mawasiliano hubadilisha matumizi yao ya lugha kulingana na muktadha, utambulisho na malengo ya mazungumzo. Data ilikusanywa nyanjani kwenye Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu. Kundi lengwa lilikuwa mawasiliano ya kesi sita ambazo zilikuwa zimeratibiwa kusikizwa katika mahakama hiyo mwezi wa Oktoba 2019. Usampulishaji wa dhamira ulitumiwa kuteua Mahakama ya Juu pamoja na kesi nne ambazo ziliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili. Mbinu ya uchunguzi usio wa kushiriki ulitumika kukusanya data. Baada ya data kukusanywa, ilipangwa na kuchanganuliwa kupitia mbinu ya uhakiki wa yaliyomo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa mawakili, hakimu, walalamishi na washtakiwa hutumia mikakati mbalimbali ya mawasiliano ambayo inaweza kuibua migogoro ya kimawasiliano au kuimarisha maelewano kati ya washiriki. Mikakati hii huwa na athari kubwa katika ufanisi wa mchakato wa maamuzi ya kesi. Makala hii inaonyesha kuwa lugha hutumiwa kama chombo muhimu cha utatuzi wa migogoro, lakini matumizi yake yanategemea sana mikakati ya mawasiliano yanayochaguliwa na washiriki. Makala hii inapendekeza kuwa, mahakama ihimize kutumiwa kwa mikakati ya mawasiliano ambayo itachochea athari chanya katika mawasiliano licha ya tofauti za kimamlaka baina ya wazungumzaji. Aidha, watafiti wa baadaye wachunguze mikakati ya mawasilano inayotumika kupitia njia ya kidijitali kwa kuwa hivi karibuni, vikao vya mahakama vinaendeshwa kupitia mitandao.
Editon Consortium Publishing
Title: Lugha, Mawasiliano na Mizozo: Mikakati ya Mawasiliano katika Kesi za Mizozo kwenye Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu
Description:
Makala hii inalenga kuchunguza mikakati ya mawasiliano inayotumika katika kesi za migogoro ya umiliki wa ardhi katika Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu.
Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Ujihusishaji iliyoasisiwa na Giles (1973) na kuendelezwa na Giles et al.
(1991).
Nadharia hii inaeleza kuwa washiriki katika mawasiliano hubadilisha matumizi yao ya lugha kulingana na muktadha, utambulisho na malengo ya mazungumzo.
Data ilikusanywa nyanjani kwenye Mahakama ya Juu ya Mazingira na Ardhi ya Jiji la Kisumu.
Kundi lengwa lilikuwa mawasiliano ya kesi sita ambazo zilikuwa zimeratibiwa kusikizwa katika mahakama hiyo mwezi wa Oktoba 2019.
Usampulishaji wa dhamira ulitumiwa kuteua Mahakama ya Juu pamoja na kesi nne ambazo ziliendeshwa kwa lugha ya Kiswahili.
Mbinu ya uchunguzi usio wa kushiriki ulitumika kukusanya data.
Baada ya data kukusanywa, ilipangwa na kuchanganuliwa kupitia mbinu ya uhakiki wa yaliyomo.
Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa mawakili, hakimu, walalamishi na washtakiwa hutumia mikakati mbalimbali ya mawasiliano ambayo inaweza kuibua migogoro ya kimawasiliano au kuimarisha maelewano kati ya washiriki.
Mikakati hii huwa na athari kubwa katika ufanisi wa mchakato wa maamuzi ya kesi.
Makala hii inaonyesha kuwa lugha hutumiwa kama chombo muhimu cha utatuzi wa migogoro, lakini matumizi yake yanategemea sana mikakati ya mawasiliano yanayochaguliwa na washiriki.
Makala hii inapendekeza kuwa, mahakama ihimize kutumiwa kwa mikakati ya mawasiliano ambayo itachochea athari chanya katika mawasiliano licha ya tofauti za kimamlaka baina ya wazungumzaji.
Aidha, watafiti wa baadaye wachunguze mikakati ya mawasilano inayotumika kupitia njia ya kidijitali kwa kuwa hivi karibuni, vikao vya mahakama vinaendeshwa kupitia mitandao.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nafasi ya Ikolojia ya Lugha katika Mtagusano wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Dini katika Kaunti ya Bungoma
Nyanja mbalimbali katika jamii hutegemea matumizi ya lugha. Hali hii huzua changamoto ya namna ya kutumia raslimali za lugha zinazopatikana katika jamiilugha fulani. Juhudi ya kufa...

