Javascript must be enabled to continue!
Raha na Karaha ya Uradidi wa Vitabu vya Fasihi kwa Shule za Sekondari Nchini Tanzania
View through CrossRef
Mihtasari ya vidato vya tatu hadi sita kupitia ujuzi wa jumla na malengo ya ufundishaji wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari nchini Tanzania, imetoa mwongozo murua kuhusu utekelezaji wake. Kwa upande wa sarufi, mambo yamenyooka si haba, kwani mwalimu ana fursa ya kutoa mifano kulingana na mazingira ya darasa lake. Changamoto inayojitokeza ni katika upande wa mada za fasihi, kwani kuna mazoea ya kujirudiarudia kwa matumizi ya vitabu vya kibunilizi: diwani, riwaya na tamthiliya, licha ya kuwapo kwa vitabu vya kutosha katika uwanja huo. Suala hilo husababisha raha na karaha katika mustakabali wa wahitimu watarajiwa. Hivyo, makala haya yamenuia kudadisi raha na karaha hizo katika ustawi wa fasihi ya Kiswahili katika jamii. Ikumbukwe kwamba wanafunzi wa leo ndio wanafasihi wa kesho katika kuzitunga, kuzihakiki na kuzichambua kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili. Kuandaliwa mazingira mazuri katika kujifunzi kutawezesha kupata wahitimu wenye uwezo wa kuhimili na kuhudumu nafasi hizo kwa weledi na uaminifu.
Title: Raha na Karaha ya Uradidi wa Vitabu vya Fasihi kwa Shule za Sekondari Nchini Tanzania
Description:
Mihtasari ya vidato vya tatu hadi sita kupitia ujuzi wa jumla na malengo ya ufundishaji wa somo la Kiswahili kwa shule za sekondari nchini Tanzania, imetoa mwongozo murua kuhusu utekelezaji wake.
Kwa upande wa sarufi, mambo yamenyooka si haba, kwani mwalimu ana fursa ya kutoa mifano kulingana na mazingira ya darasa lake.
Changamoto inayojitokeza ni katika upande wa mada za fasihi, kwani kuna mazoea ya kujirudiarudia kwa matumizi ya vitabu vya kibunilizi: diwani, riwaya na tamthiliya, licha ya kuwapo kwa vitabu vya kutosha katika uwanja huo.
Suala hilo husababisha raha na karaha katika mustakabali wa wahitimu watarajiwa.
Hivyo, makala haya yamenuia kudadisi raha na karaha hizo katika ustawi wa fasihi ya Kiswahili katika jamii.
Ikumbukwe kwamba wanafunzi wa leo ndio wanafasihi wa kesho katika kuzitunga, kuzihakiki na kuzichambua kazi mbalimbali za fasihi ya Kiswahili.
Kuandaliwa mazingira mazuri katika kujifunzi kutawezesha kupata wahitimu wenye uwezo wa kuhimili na kuhudumu nafasi hizo kwa weledi na uaminifu.
Related Results
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Utata wa Maudhui ya Kisarufi katika Vitabu vya Kiada vya Kiswahili Kidato cha Kwanza na cha Tatu Nchini Tanzania
Vitabu vya kiada ni nyenzo muhimu katika ufundishaji wa somo la Kiswahili nchini Tanzania. Hutumika kama mwongozo wa ufundishaji wa mada zilizoteuliwa kwa kiwango husika cha elimu....
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Mikabala Mbalimbali ya Uchanganuzi wa Sentensi Changamano za Kiswahili katika Vitabu vya Kiada vya Shule za Sekondari
Rasimu ya mtalaa mpya wa elimu nchini Kenya imebaini vipengele anavyopaswa kuzingatishwa mwanafunzi ili kuimarisha uwezo na maarifa yake katika ujifunzaji wa Kiswahili. Hali hii im...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu