Javascript must be enabled to continue!
Kuwezeshwa kwa uchumi kupitia lugha ya kiswahili
View through CrossRef
Makala haya yanalenga kuangazia juhudi za nchi za Afrika mashariki na bara la Afrika kutumia Kiswahili kama nyenzo ya mawasiliono miongoni mwao ili kurahisisha mawasiliano na biashara kati ya wananchi wa mataifa haya. Makala haya yametumia data za kimsingi za tafiti za awali katika kufikia hitimisho lake. Lugha nyingine zinazozungumzwa Afrika masharika kando na lugha-mame za wazaliwa wa Afrika mashariki ni, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani. Lugha hizi zilizokuja na mkoloni pia zimepata nafasi kubwa katika jamii ya Afrika kwa ujumla. Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la matumizi ya lugha ya Kichina na mafunzo kutolewa kwa waafrika kwa lugha hii. Hata hivyo, lugha hizi zinaendelezwa kwa mtazamo na imani za waafrika wenyewe. Waafrika wengi wanaamini kuwa, maendeleo na kungeuka kunatokana na lugha hizi za kikoloni. Mitazamo hii ni tata na imelifanya bara la Afrika kuyumba kimaendeleo. Baadhi ya nchi za Afrika zinatumia lugha za kikoloni kama lugha zao rasmi. Hili linalazimisha yeyote anayezuru nchi hizi ajifunze lugha yao ili kuwepo mawasiliano. Hatua zinazochukulia na nchi za Afrika kutafuta lugha ya kutumika katika nchi zote Afrika ni juhudi za kupewa nguvu na kuungwa mkono na kila nchi ya Afrika. maendeleo hutegemea mawasiliano bora na ambayo hufanikishwa na lugha. Kiswahili kuwa lugha yenye asili ya Kiafrika na juhudi hizi za maenezi kutoka kwa nchi za kiafrika basi itakuwa kiunganishi bora cha nchi hizi.
Title: Kuwezeshwa kwa uchumi kupitia lugha ya kiswahili
Description:
Makala haya yanalenga kuangazia juhudi za nchi za Afrika mashariki na bara la Afrika kutumia Kiswahili kama nyenzo ya mawasiliono miongoni mwao ili kurahisisha mawasiliano na biashara kati ya wananchi wa mataifa haya.
Makala haya yametumia data za kimsingi za tafiti za awali katika kufikia hitimisho lake.
Lugha nyingine zinazozungumzwa Afrika masharika kando na lugha-mame za wazaliwa wa Afrika mashariki ni, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani.
Lugha hizi zilizokuja na mkoloni pia zimepata nafasi kubwa katika jamii ya Afrika kwa ujumla.
Siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la matumizi ya lugha ya Kichina na mafunzo kutolewa kwa waafrika kwa lugha hii.
Hata hivyo, lugha hizi zinaendelezwa kwa mtazamo na imani za waafrika wenyewe.
Waafrika wengi wanaamini kuwa, maendeleo na kungeuka kunatokana na lugha hizi za kikoloni.
Mitazamo hii ni tata na imelifanya bara la Afrika kuyumba kimaendeleo.
Baadhi ya nchi za Afrika zinatumia lugha za kikoloni kama lugha zao rasmi.
Hili linalazimisha yeyote anayezuru nchi hizi ajifunze lugha yao ili kuwepo mawasiliano.
Hatua zinazochukulia na nchi za Afrika kutafuta lugha ya kutumika katika nchi zote Afrika ni juhudi za kupewa nguvu na kuungwa mkono na kila nchi ya Afrika.
maendeleo hutegemea mawasiliano bora na ambayo hufanikishwa na lugha.
Kiswahili kuwa lugha yenye asili ya Kiafrika na juhudi hizi za maenezi kutoka kwa nchi za kiafrika basi itakuwa kiunganishi bora cha nchi hizi.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Umuhimu Wa Kufundisha Lugha Ya Kiswahili Katika Shule Za Sekondari Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza namna ambavyo Kiswahili kinaweza kuwa na manufaa kwa nchi ya Uganda. Ni kweli kwamba nchini Uganda, watu kadhaa wakiwemo baadhi ya wanasiasa ha...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili
Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Kuchambua Athari ya Vivumishi vya Runyakitara Katika Ujifunzaji wa Lugha ya Kiswahili Nchini Uganda
Katika mfumo wa elimu nchini Uganda, Kiswahili ni lugha muhimu kwa mawasiliano na maendeleo ya kijamii. Hata hivyo, wanafunzi wanaozungumza Runyakitara wanakumbana na changamoto ka...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...

