Javascript must be enabled to continue!
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
View through CrossRef
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti alieleza namna wazazi wanavyotumia lugha kulea watoto wao. Alifanya hivyo kwa kunukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana zinatumiwa na wazazi katika shughuli ya kulea watoto. Ni kweli kwamba lugha yoyote ile hufanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kuficha siri, kuseng’enya watu, kuibia watu, kutongozana, kushawishi, kugombana, kujitetea, kufundisha, nakadhalika. Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba, akagombana, akaiba kwa kudang’anya, akafundisha, akaseng’enya, akatongoza, n.k. Hata hivyo, katika makala haya, mtafiti alijikita kwenye malezi ya watoto. Katika kazi hii, mtafiti alizingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuwaelekeza watoto wao ili wasije wakatenda maovu ukubwani. Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili. Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuwaelekeza watoto wao. Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza watoto wao. Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa. Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo. Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto. Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza watoto wenye tabia nzuri. Hii ni kwa sababu watoto wenye tabia mbaya waliletea wazazi wao aibu. Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti alijikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza watoto wao kitabia.
East African Nature and Science Organization
Title: Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Description:
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto.
Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda.
Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti alieleza namna wazazi wanavyotumia lugha kulea watoto wao.
Alifanya hivyo kwa kunukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana zinatumiwa na wazazi katika shughuli ya kulea watoto.
Ni kweli kwamba lugha yoyote ile hufanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kuficha siri, kuseng’enya watu, kuibia watu, kutongozana, kushawishi, kugombana, kujitetea, kufundisha, nakadhalika.
Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba, akagombana, akaiba kwa kudang’anya, akafundisha, akaseng’enya, akatongoza, n.
k.
Hata hivyo, katika makala haya, mtafiti alijikita kwenye malezi ya watoto.
Katika kazi hii, mtafiti alizingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuwaelekeza watoto wao ili wasije wakatenda maovu ukubwani.
Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili.
Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuwaelekeza watoto wao.
Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza watoto wao.
Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa.
Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo.
Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto.
Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza watoto wenye tabia nzuri.
Hii ni kwa sababu watoto wenye tabia mbaya waliletea wazazi wao aibu.
Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti alijikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza watoto wao kitabia.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...


