Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda

View through CrossRef
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwango cha umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari kilikuwa cha chini sana licha ya kufundishwa lugha hiyo kwa kutumia Mtaala wa Maarifa. Utafiti wa awali uliofanywa na watafiti ulibainisha kuwa, kiwango cha umahiri cha wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili kimeongezeka tangu kuanza kutumiwa kwa Mtaala wa Umilisi katika ufundishaji mwaka 2020 tofauti na ilivyokuwa chini ya Mtaala wa Maarifa. Kutokana na matokeo hayo, utafiti uliozaa makala haya umetathmini athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda. Sampuli ya watoataarifa kumi na wawili (12) walimu na ishirini na wanne (24) wanafunzi ilitumika kwenye utafiti huu. Nadharia ya Mawasiliano katika Ufundishaji wa Lugha imetumika katika uchanganuzi wa data za utafiti. Mbinu zilizotumika kukusanya data za utafiti huu ni ushuhudiaji na usaili. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba, athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili imebainika kuwa mtaala una athari chanya. Athari hizo zipo katika mbinu za ufundishaji, mbinu za ujifunzaji, mawanda ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi husika na mawanda ya ujifunzaji na tathmini.
Title: Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Description:
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili.
Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwango cha umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari kilikuwa cha chini sana licha ya kufundishwa lugha hiyo kwa kutumia Mtaala wa Maarifa.
Utafiti wa awali uliofanywa na watafiti ulibainisha kuwa, kiwango cha umahiri cha wanafunzi kuzungumza lugha ya Kiswahili kimeongezeka tangu kuanza kutumiwa kwa Mtaala wa Umilisi katika ufundishaji mwaka 2020 tofauti na ilivyokuwa chini ya Mtaala wa Maarifa.
Kutokana na matokeo hayo, utafiti uliozaa makala haya umetathmini athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Uganda.
Sampuli ya watoataarifa kumi na wawili (12) walimu na ishirini na wanne (24) wanafunzi ilitumika kwenye utafiti huu.
Nadharia ya Mawasiliano katika Ufundishaji wa Lugha imetumika katika uchanganuzi wa data za utafiti.
Mbinu zilizotumika kukusanya data za utafiti huu ni ushuhudiaji na usaili.
Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba, athari za Mtaala wa Umilisi katika ukuzaji wa umahiri wa kuzungumza Kiswahili imebainika kuwa mtaala una athari chanya.
Athari hizo zipo katika mbinu za ufundishaji, mbinu za ujifunzaji, mawanda ya matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi husika na mawanda ya ujifunzaji na tathmini.

Related Results

Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, ut...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...

Back to Top