Javascript must be enabled to continue!
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
View through CrossRef
Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi. Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho kinapaswa kuwa kiima na sio kiambajengo kilichopo katika nafsi ya chini. Tungo zenye upinduzi wa kimahali zinakiuka uhusiano huo. Katika tungo hizo, kimahali, ambacho kipo katika nafasi ya chini, kinakuwa kiima ilihali sio mtenda au kithimu. Wataalamu mbalimbali wamefafanua tungo hizi katika lugha za Kibantu. Licha ya kufanya hivyo, hakuna uwazi kuhusu sifa za muundo wa taarifa na sababu za upinduzi wa kimahali katika mawasiliano. Hivyo, makala haya yanafafanua na kubainisha masuala hayo katika lugha ya Kiswahili. Data zilizotumika zimepatikana kwa mbinu ya uchambuzi wa matini, upimaji wa usahihi wa kisarufi pamoja na usaili. Data hizo zimefasiriwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Sarufi Leksia Amilifu (Bresnan na Kaplan, 1982). Baada ya kufasiri data hizo, makala haya yanabainisha kwamba muundo wa taarifa wa tungo hizi una aina mbili za taarifa, yaani mada na fokasi. Aidha, makala yanafafanua kwamba upinduzi wa kimahali unatokea kwa sababu ya umadaishaji wa kimahali na ufokalishaji wa kithimu/mtenda.
Title: Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Description:
Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi.
Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho kinapaswa kuwa kiima na sio kiambajengo kilichopo katika nafsi ya chini.
Tungo zenye upinduzi wa kimahali zinakiuka uhusiano huo.
Katika tungo hizo, kimahali, ambacho kipo katika nafasi ya chini, kinakuwa kiima ilihali sio mtenda au kithimu.
Wataalamu mbalimbali wamefafanua tungo hizi katika lugha za Kibantu.
Licha ya kufanya hivyo, hakuna uwazi kuhusu sifa za muundo wa taarifa na sababu za upinduzi wa kimahali katika mawasiliano.
Hivyo, makala haya yanafafanua na kubainisha masuala hayo katika lugha ya Kiswahili.
Data zilizotumika zimepatikana kwa mbinu ya uchambuzi wa matini, upimaji wa usahihi wa kisarufi pamoja na usaili.
Data hizo zimefasiriwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Sarufi Leksia Amilifu (Bresnan na Kaplan, 1982).
Baada ya kufasiri data hizo, makala haya yanabainisha kwamba muundo wa taarifa wa tungo hizi una aina mbili za taarifa, yaani mada na fokasi.
Aidha, makala yanafafanua kwamba upinduzi wa kimahali unatokea kwa sababu ya umadaishaji wa kimahali na ufokalishaji wa kithimu/mtenda.
Related Results
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...

