Javascript must be enabled to continue!
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
View through CrossRef
Ikisiri
Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na umuhimu wake mkubwa katika lugha na mawasiliano kwa ujumla. Umuhimu huo ni kutambulisha watu, vitu, hali na mahali. Gᴉrᴉmi, kutokana na utangamano wake na Kiswahili, kinakopa na kutohoa nomino tofauti kwa lengo la kukidhi mawasiliano kulingana na wakati na mazingira ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii yanayoikabili lugha hiyo. Uchambuzi matini na usaili vimeonesha kwamba nomino za Kiswahili zinazokopwa na kupokelewa katika Gᴉrᴉmi ni za ngeli nane ambazo ni MU-/WA-; MU-/MI-; JI-, Ø-/MA-; KI-/VI-; N-/N-; U-/N-; U-/MA-; na KU-, ambapo maumbo ya umoja na wingi, pamoja na sauti huchakatwa kulingana na mfumo lugha wa Gᴉrᴉmi. Hata hivyo, maana ya nomino inayokopwa hubaki ileile kama ilivyo katika lugha iliyokopesha. Kwa hiyo, inapendekezwa uchambuzi wowote wa mapokezi ya maneno uende sambamba na mfumo wa lugha inayokopa.
Title: Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Description:
Ikisiri
Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi.
Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na umuhimu wake mkubwa katika lugha na mawasiliano kwa ujumla.
Umuhimu huo ni kutambulisha watu, vitu, hali na mahali.
Gᴉrᴉmi, kutokana na utangamano wake na Kiswahili, kinakopa na kutohoa nomino tofauti kwa lengo la kukidhi mawasiliano kulingana na wakati na mazingira ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii yanayoikabili lugha hiyo.
Uchambuzi matini na usaili vimeonesha kwamba nomino za Kiswahili zinazokopwa na kupokelewa katika Gᴉrᴉmi ni za ngeli nane ambazo ni MU-/WA-; MU-/MI-; JI-, Ø-/MA-; KI-/VI-; N-/N-; U-/N-; U-/MA-; na KU-, ambapo maumbo ya umoja na wingi, pamoja na sauti huchakatwa kulingana na mfumo lugha wa Gᴉrᴉmi.
Hata hivyo, maana ya nomino inayokopwa hubaki ileile kama ilivyo katika lugha iliyokopesha.
Kwa hiyo, inapendekezwa uchambuzi wowote wa mapokezi ya maneno uende sambamba na mfumo wa lugha inayokopa.
Related Results
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, ut...
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi. Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho kinapa...