Javascript must be enabled to continue!
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
View through CrossRef
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambishi ngeli {m-/mu-, ji-, ma-, ki-, ka-, tu, na u-} katika nomino hizi unaathiri sifa tajwa. Makala haya yanafafanua athari za kimofolojia na za kisemantiki za uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino hizi na maana ya athari hizo katika ufafanuzi wa sarufi ya Kiswahili. Data zilizotumika zilipatikana kwa njia ya ushuhudiaji shiriki, hojaji na usaili. Data hizo zilifafanuliwa kwa kutumia Nadharia ya Matumizi iliyoasisiwa na Lodwig Wittgenstein (1953). Kutokana na data hizo, makala yanaonesha kwamba uambikaji wa viambishi ngeli kwenye nomino hizi husababisha athari za kimofolojia kama vile kuongeza idadi ya mofu kutoka moja kuwa mbili na kubadili aina ya nomino kimuundo. Vilevile, uambikaji huo huathiri maana ya nomino hizo kisarufi na kileksika kwa kuzingatia matumizi yake. Iwapo nomino hizi zitaendelea kupata mashiko na kisha kusanifiwa, athari tajwa zinadokeza mahitaji ya kuboresha uainishaji wa ngeli za nomino, uandikaji wa taarifa za vidahizo katika kamusi na ufafanuzi wa upanuzi na mabadiliko ya maana katika sarufi ya Kiswahili. Hivyo, imehitimishwa kwamba athari za kimofolojia na kisemantiki zinazotokana na uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino sahili zinadhihirisha mabadiliko ya lugha na kwamba mabadiliko haya yanapaswa kuzingatiwa katika ufafanuzi wa sarufi ya Kiswahili. Kutokana na matokeo haya, imependekezwa kwamba zifanyike tafiti kuhusu uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino sahili za makundi mengine ya nomino katika lugha ya Kiswahili.
Title: Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Description:
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja.
Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi.
Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambishi ngeli {m-/mu-, ji-, ma-, ki-, ka-, tu, na u-} katika nomino hizi unaathiri sifa tajwa.
Makala haya yanafafanua athari za kimofolojia na za kisemantiki za uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino hizi na maana ya athari hizo katika ufafanuzi wa sarufi ya Kiswahili.
Data zilizotumika zilipatikana kwa njia ya ushuhudiaji shiriki, hojaji na usaili.
Data hizo zilifafanuliwa kwa kutumia Nadharia ya Matumizi iliyoasisiwa na Lodwig Wittgenstein (1953).
Kutokana na data hizo, makala yanaonesha kwamba uambikaji wa viambishi ngeli kwenye nomino hizi husababisha athari za kimofolojia kama vile kuongeza idadi ya mofu kutoka moja kuwa mbili na kubadili aina ya nomino kimuundo.
Vilevile, uambikaji huo huathiri maana ya nomino hizo kisarufi na kileksika kwa kuzingatia matumizi yake.
Iwapo nomino hizi zitaendelea kupata mashiko na kisha kusanifiwa, athari tajwa zinadokeza mahitaji ya kuboresha uainishaji wa ngeli za nomino, uandikaji wa taarifa za vidahizo katika kamusi na ufafanuzi wa upanuzi na mabadiliko ya maana katika sarufi ya Kiswahili.
Hivyo, imehitimishwa kwamba athari za kimofolojia na kisemantiki zinazotokana na uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino sahili zinadhihirisha mabadiliko ya lugha na kwamba mabadiliko haya yanapaswa kuzingatiwa katika ufafanuzi wa sarufi ya Kiswahili.
Kutokana na matokeo haya, imependekezwa kwamba zifanyike tafiti kuhusu uambikaji wa viambishi ngeli katika nomino sahili za makundi mengine ya nomino katika lugha ya Kiswahili.
Related Results
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Ikisiri
Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, ut...
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Utafiti huu unalenga kupambanua kanuni zinazotawala mageuzi katika sentensi sahili ya Ekegusii language in Kenya. Nadharia ya Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo uliongoza uta...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...

