Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ishara na Uashiriaji kama Mikakati ya Uchimuzi katika Riwaya za Maundu Mwingizi

View through CrossRef
Makala hii inachanganua ishara na uashiriaji kama mkakati wa uchimuzi katika riwaya za Vita vya Mapenzi (2012), Mzimu wa Waufi (2013), na Tanzia (2015) za Maundu Mwingizi. Tatizo lililochochea utafiti huu ni kuwepo kwa pengo la kitaaluma katika uchambuzi wa ishara na uashiriaji kama mkakati wa uchimuzi wa maudhui katika riwaya hizi. Hivyo, utafiti ulilenga kuchanganua matumizi ya ishara na uashiriaji katika kuchimuza maudhui mbalimbali. Makala hii imejikita katika nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Saussure (1916), ambapo ishara huundwa na kitaja (signifier) na kitajwa (signified), ambavyo vilitumika kama msingi wa uchambuzi wa data. Utafiti ulikuwa wa maktabani na ulitumia mkabala wa kimaelezo. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya teule, huku data zikichanganuliwa kwa mbinu ya uchanganuzi wa matini na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yalibaini kuwa mtunzi ametumia kwa ustadi ishara bia na zisizo bia, zikiwemo pete, rangi na mazingira, kuchimuza maudhui mbalimbali katika miktadha halisia na ya kihalisiajabu yenye matukio ya kutisha na kuogofya. Aidha, ilibainika kuwa ishara hizo zimeibuliwa kutoka katika visasili, historia na mitazamo ya kimaadili ili kuwasilisha ujumbe kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kwa kutumia mtindo wa uhalisiamazingaombwe. Utafiti unahitimisha kuwa ishara na uashiriaji ni mbinu muhimu za kisanaa zinazomwezesha Maundu Mwingizi kuchimuza maudhui kwa kina na kuchochea tafakuri kwa msomaji. Utafiti unapendekeza tafiti zaidi kuhusu matumizi ya ishara na uashiriaji katika kazi nyingine za fasihi ya Kiswahili kwa kutumia nadharia mbalimbali.
Title: Ishara na Uashiriaji kama Mikakati ya Uchimuzi katika Riwaya za Maundu Mwingizi
Description:
Makala hii inachanganua ishara na uashiriaji kama mkakati wa uchimuzi katika riwaya za Vita vya Mapenzi (2012), Mzimu wa Waufi (2013), na Tanzia (2015) za Maundu Mwingizi.
Tatizo lililochochea utafiti huu ni kuwepo kwa pengo la kitaaluma katika uchambuzi wa ishara na uashiriaji kama mkakati wa uchimuzi wa maudhui katika riwaya hizi.
Hivyo, utafiti ulilenga kuchanganua matumizi ya ishara na uashiriaji katika kuchimuza maudhui mbalimbali.
Makala hii imejikita katika nadharia ya Semiotiki iliyoasisiwa na Saussure (1916), ambapo ishara huundwa na kitaja (signifier) na kitajwa (signified), ambavyo vilitumika kama msingi wa uchambuzi wa data.
Utafiti ulikuwa wa maktabani na ulitumia mkabala wa kimaelezo.
Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya teule, huku data zikichanganuliwa kwa mbinu ya uchanganuzi wa matini na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Matokeo yalibaini kuwa mtunzi ametumia kwa ustadi ishara bia na zisizo bia, zikiwemo pete, rangi na mazingira, kuchimuza maudhui mbalimbali katika miktadha halisia na ya kihalisiajabu yenye matukio ya kutisha na kuogofya.
Aidha, ilibainika kuwa ishara hizo zimeibuliwa kutoka katika visasili, historia na mitazamo ya kimaadili ili kuwasilisha ujumbe kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii kwa kutumia mtindo wa uhalisiamazingaombwe.
Utafiti unahitimisha kuwa ishara na uashiriaji ni mbinu muhimu za kisanaa zinazomwezesha Maundu Mwingizi kuchimuza maudhui kwa kina na kuchochea tafakuri kwa msomaji.
Utafiti unapendekeza tafiti zaidi kuhusu matumizi ya ishara na uashiriaji katika kazi nyingine za fasihi ya Kiswahili kwa kutumia nadharia mbalimbali.

Related Results

Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Upambanuzi wa Mikakati ya Kitashtiti katika Vibonzo vya Kisiasa Vya Gado
Taalumu ya uchoraji na uchapishaji wa vibonzo vya kisiasa umekuwepo tangu karne ya kumi na nane. Saana hii huwavutia watafiti wengi kutokana na uwezo wake wa kusimba jumbe zisizowe...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo. Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikis...
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi san...

Back to Top