Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili

View through CrossRef
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanywa kuhusu methali za Kiswahili. Tafiti hizo zimejikita mno kwenye fasiri za maana, fafanuzi, uainishaji na maelezo ya kijumla. Juhudi hizo za awali zinaashiria kuwa, methali za Kiswahili ni ‘jungu kuu’ na zinahitaji uhakiki na utafiti wa kina. Kutokana na umuhimu wake katika jamii, zimekuwa zikipokezwa kimuktadha kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa maana hii, zimekuwa ni vito vya kuhifadhi na kuwasilisha busara zinazojikita katika falsafa za jamii. Aidha, zimekuwa zikitumika zaidi katika ubainishaji na uelekezaji wa masuala muhimu ya jamii. Maelezo ya kijumla yamekuwa yakitolewa kuhusu methali hizo kwamba, ni ‘kauli fupi’ za kimapokeo. Huo ni uegemeo unaojikita kwenye sifa za kimuundo na kimaumbo. Mwelekeo huo hausaidii sana katika ubainishaji wa busara katika jamii husika. Kutokana na jinsi methali za Kiswahili zinavyotumiwa katika jamii, kuna namna mbili zinazojitokeza: ufupi na urefu wake. Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kufafanulia sura hizo mbili kwa kuzingatia miktadha ya kijamii.
University of Dar es Salaam
Title: Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili
Description:
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanywa kuhusu methali za Kiswahili.
Tafiti hizo zimejikita mno kwenye fasiri za maana, fafanuzi, uainishaji na maelezo ya kijumla.
Juhudi hizo za awali zinaashiria kuwa, methali za Kiswahili ni ‘jungu kuu’ na zinahitaji uhakiki na utafiti wa kina.
Kutokana na umuhimu wake katika jamii, zimekuwa zikipokezwa kimuktadha kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Kwa maana hii, zimekuwa ni vito vya kuhifadhi na kuwasilisha busara zinazojikita katika falsafa za jamii.
Aidha, zimekuwa zikitumika zaidi katika ubainishaji na uelekezaji wa masuala muhimu ya jamii.
Maelezo ya kijumla yamekuwa yakitolewa kuhusu methali hizo kwamba, ni ‘kauli fupi’ za kimapokeo.
Huo ni uegemeo unaojikita kwenye sifa za kimuundo na kimaumbo.
Mwelekeo huo hausaidii sana katika ubainishaji wa busara katika jamii husika.
Kutokana na jinsi methali za Kiswahili zinavyotumiwa katika jamii, kuna namna mbili zinazojitokeza: ufupi na urefu wake.
Nadharia ya Semiotiki imetumika katika kufafanulia sura hizo mbili kwa kuzingatia miktadha ya kijamii.

Related Results

Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Dhima ya Methali Kinzani
Dhima ya Methali Kinzani
Maadili katika jamii ni kipengele muhimu cha utamaduni na aghalabu huwasilishwa kupitia methali. Kimsingi, methali ni kauli za kifalsafa zinazotumiwa kuelezea na kuelekezea masuala...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...

Back to Top