Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Dhima ya Methali Kinzani

View through CrossRef
Maadili katika jamii ni kipengele muhimu cha utamaduni na aghalabu huwasilishwa kupitia methali. Kimsingi, methali ni kauli za kifalsafa zinazotumiwa kuelezea na kuelekezea masuala kuhusu maisha ya wanajamii. Watu wanapozungumza, methali hujitokeza kama matini za ndani kwa ndani. Hivyo, methali hubeba ujumbe wa jumla unaohitaji kupatanishwa na miktadha ya kijamii. Mazingira haya huakisi mtazamo na tajiriba za jamii. Methali zinapotumiwa, huwa kurunzi ya kuukoleza zaidi ujumbe. Zinapotumika katika mazungumzo, matarajio ni kuibua jibu au tendo; kuonya kwa kuzingatia utamaduni wa jamii; kusuta matendo na kukemea matendo hasi ya watu. Katika uelekezaji wa maadili katika jamii, methali hutoa maelezo au kusuta kwa kuzingatia misimamo ‘mikali’. Methali hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa ujumla kuwa zinapingana na zina mwelekeo hasi. Makala haya yanahakiki dhima ya methali kinzani katika kubainishia zaidi ujumbe wa kimaadili. Aidha, inabainishwa kuwa, methali zaidi ya moja zinaweza kutumiwa katika uwasilishaji wa ujumbe wa jumla na uelekezaji wa maadili katika jamii. Methali kinzani ni msingi katika kujengea mazingira ya uwajibikaji binafsi au wa kikundi cha watu.
University of Dar es Salaam
Title: Dhima ya Methali Kinzani
Description:
Maadili katika jamii ni kipengele muhimu cha utamaduni na aghalabu huwasilishwa kupitia methali.
Kimsingi, methali ni kauli za kifalsafa zinazotumiwa kuelezea na kuelekezea masuala kuhusu maisha ya wanajamii.
Watu wanapozungumza, methali hujitokeza kama matini za ndani kwa ndani.
Hivyo, methali hubeba ujumbe wa jumla unaohitaji kupatanishwa na miktadha ya kijamii.
Mazingira haya huakisi mtazamo na tajiriba za jamii.
Methali zinapotumiwa, huwa kurunzi ya kuukoleza zaidi ujumbe.
Zinapotumika katika mazungumzo, matarajio ni kuibua jibu au tendo; kuonya kwa kuzingatia utamaduni wa jamii; kusuta matendo na kukemea matendo hasi ya watu.
Katika uelekezaji wa maadili katika jamii, methali hutoa maelezo au kusuta kwa kuzingatia misimamo ‘mikali’.
Methali hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa ujumla kuwa zinapingana na zina mwelekeo hasi.
Makala haya yanahakiki dhima ya methali kinzani katika kubainishia zaidi ujumbe wa kimaadili.
Aidha, inabainishwa kuwa, methali zaidi ya moja zinaweza kutumiwa katika uwasilishaji wa ujumbe wa jumla na uelekezaji wa maadili katika jamii.
Methali kinzani ni msingi katika kujengea mazingira ya uwajibikaji binafsi au wa kikundi cha watu.

Related Results

Maarifa ya Kiikolojia na Kijamii kutoka katika Methali za Kiswahili Zinazotaja Mimea
Maarifa ya Kiikolojia na Kijamii kutoka katika Methali za Kiswahili Zinazotaja Mimea
Methali ni kipera cha fasihi simulizi kinachopatikana katika utanzu wa semi. Methali husheheni maarifa mbalimbali yenye kuifaa jamii husika. Lengo la makala hii ni kujadili maarifa...
Iktibasi katika Methali za Waswahili
Iktibasi katika Methali za Waswahili
Makala hii inalenga kuchunguza namna iktibasi inavyojitokeza katika methali za Waswahili. Iktibasi ni dhana ya Kiarabu kwa mujibu wa Karisa na Mwinyifaki (2013). Ni mbinu ya kuchot...
Ala za Kisintaksia katika Ufafanuzi wa Dhima za Viambajengo vya katika Lugha ya Kiswahili
Ala za Kisintaksia katika Ufafanuzi wa Dhima za Viambajengo vya katika Lugha ya Kiswahili
Makala hii inahusu ala za sintaksia na namna ambavyo zinaweza kutumika katika ufafanuzi wa dhima za kisarufi za viambajengo vya sentensi za lugha ya Kiswahili. Licha ya ufafanuzi w...
Dhima ya Ngoma katika Tamthiliya ya Kiswahili ya Kimajaribio: Mfano kutoka Lina Ubani (1984)
Dhima ya Ngoma katika Tamthiliya ya Kiswahili ya Kimajaribio: Mfano kutoka Lina Ubani (1984)
Makala hii inachunguza dhima ya ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio. Tafiti kuhusu matumizi ya ngoma katika tamthiliya ya Kiswahili ya kimajaribio zimeishia katika ...
Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili
Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanywa kuhusu methali za Kiswahili. Tafiti hizo zimejikita mno kwenye fasiri za maana, fafanuzi, uainishaji na maelezo ya kijumla. Juhudi hizo za awali...
Dhima ya Kialami Pragmatiki ‘Hivi’ katika Mawasiliano ya Kiswahili
Dhima ya Kialami Pragmatiki ‘Hivi’ katika Mawasiliano ya Kiswahili
Makala hii inahusu dhima za kialami pragmatiki hivi katika mawasiliano ya Kiswahili. Data za makala hii zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yanayofanywa katika vijiwe vya mamalis...
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Mchango wa Ujumi Mweusi katika Unusura wa Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania: 1970- 2000
Nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania zilianza nchini Tanzania kipindi cha ukoloni. Nyimbo hizi zinasawiri ujumi mweusi kwa kiasi kikubwa, na zina unusura. Ujumi wa kijamii huwa na...

Back to Top