Javascript must be enabled to continue!
Iktibasi katika Methali za Waswahili
View through CrossRef
Makala hii inalenga kuchunguza namna iktibasi inavyojitokeza katika methali za Waswahili. Iktibasi ni dhana ya Kiarabu kwa mujibu wa Karisa na Mwinyifaki (2013). Ni mbinu ya kuchota mafundisho ya Kurani Tukufu na Sunnah na kuyatumia katika fasihi bila kuonesha yametoka katika Kurani Tukufu na Sunnah (Karisa na Mwinyifaki, 2013). Maisha ya Waswahili licha ya kuongozwa na maadili yaliyomo katika mafundisho ya dini ya Kiislamu, methali zinazotumiwa na Waswahili hao katika mazungumzo yao ya kila siku pia huchangia kutilia nguvu mafundisho ya dini. Uchunguzi huu umechochewa na methali za jamii ya Waswahili ambazo zinaelekea kusheheni mafundisho ya dini. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uislamu kwa mujibu wa mawazo ya Hashi (2011) katika kubainisha namna mafundisho ya Kurani na Hadith yanavyojitokeza katika methali za Waswahili. Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba methali za Waswahili zilisheheni mafundisho ya maadili ambayo yalipatikana pia katika Kurani na Hadith. Uhusiano mwema kati ya binadamu na binadamu na binadamu na Mungu unapatikana katika methali, na Kurani na Hadith vilevile.
Title: Iktibasi katika Methali za Waswahili
Description:
Makala hii inalenga kuchunguza namna iktibasi inavyojitokeza katika methali za Waswahili.
Iktibasi ni dhana ya Kiarabu kwa mujibu wa Karisa na Mwinyifaki (2013).
Ni mbinu ya kuchota mafundisho ya Kurani Tukufu na Sunnah na kuyatumia katika fasihi bila kuonesha yametoka katika Kurani Tukufu na Sunnah (Karisa na Mwinyifaki, 2013).
Maisha ya Waswahili licha ya kuongozwa na maadili yaliyomo katika mafundisho ya dini ya Kiislamu, methali zinazotumiwa na Waswahili hao katika mazungumzo yao ya kila siku pia huchangia kutilia nguvu mafundisho ya dini.
Uchunguzi huu umechochewa na methali za jamii ya Waswahili ambazo zinaelekea kusheheni mafundisho ya dini.
Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uislamu kwa mujibu wa mawazo ya Hashi (2011) katika kubainisha namna mafundisho ya Kurani na Hadith yanavyojitokeza katika methali za Waswahili.
Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba methali za Waswahili zilisheheni mafundisho ya maadili ambayo yalipatikana pia katika Kurani na Hadith.
Uhusiano mwema kati ya binadamu na binadamu na binadamu na Mungu unapatikana katika methali, na Kurani na Hadith vilevile.
Related Results
Dhima ya Methali Kinzani
Dhima ya Methali Kinzani
Maadili katika jamii ni kipengele muhimu cha utamaduni na aghalabu huwasilishwa kupitia methali. Kimsingi, methali ni kauli za kifalsafa zinazotumiwa kuelezea na kuelekezea masuala...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Maarifa ya Kiikolojia na Kijamii kutoka katika Methali za Kiswahili Zinazotaja Mimea
Maarifa ya Kiikolojia na Kijamii kutoka katika Methali za Kiswahili Zinazotaja Mimea
Methali ni kipera cha fasihi simulizi kinachopatikana katika utanzu wa semi. Methali husheheni maarifa mbalimbali yenye kuifaa jamii husika. Lengo la makala hii ni kujadili maarifa...
Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili
Ubainishaji wa ‘Sura Mbili’ katika Methali za Kiswahili
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanywa kuhusu methali za Kiswahili. Tafiti hizo zimejikita mno kwenye fasiri za maana, fafanuzi, uainishaji na maelezo ya kijumla. Juhudi hizo za awali...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...

