Javascript must be enabled to continue!
Utenge wa tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili katika mabango yaliyopo Barabara Kuu ya Moshi – Arusha
View through CrossRef
Katika Barabara Kuu ya Moshi-Arusha, eneo la Usa River, kuna mabango anuwai ambayo yanalenga kutangaza biashara na shughuli zinazofanywa na asasi na watu binafsi. Kutokana na mwingiliano wa watu wanaotumia barabara hii, mabango haya yamelazimika kutumia uwililugha1, yaani Kiingereza na Kiswahili. Uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye mabango mengi yaliyopo katika barabara hiyo umebaini kuwa, mbali na mambo mengine, utenge wa wazi katika tafsiri zilizomo katika mabango hayo. Hicho ndicho kilichotuchochea kufanya utafiti ulioibua makala hii. Jumla ya mabango 30 yalikusanywa kwa njia ya kupiga picha, kisha uchambuzi wa kimaudhui ulifanyika kuhusu mabango hayo. Kwa hiyo, makala hii inabainisha makosa ya tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwenye mabango hayo. Jumla ya mabango 30 yalitumika kama data. Kwa kuongozwa na misingi ya Nadharia ya Usawe wa Kidhima, tulibainisha dosari mbalimbali za tafsiri zilizojidhihirisha katika mabango hayo. Makosa yaliyobainishwa ni: makosa ya kisemantiki, makosa ya kimofolojia, makosa ya ki-tafsiri na makosa ya kisintaksia. Makala imehitimishwa kwa kugusia vipengele vinavyoweza kuzingatiwa ili kupunguza dosari hizo.
African Journals Online (AJOL)
Title: Utenge wa tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili katika mabango yaliyopo Barabara Kuu ya Moshi – Arusha
Description:
Katika Barabara Kuu ya Moshi-Arusha, eneo la Usa River, kuna mabango anuwai ambayo yanalenga kutangaza biashara na shughuli zinazofanywa na asasi na watu binafsi.
Kutokana na mwingiliano wa watu wanaotumia barabara hii, mabango haya yamelazimika kutumia uwililugha1, yaani Kiingereza na Kiswahili.
Uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye mabango mengi yaliyopo katika barabara hiyo umebaini kuwa, mbali na mambo mengine, utenge wa wazi katika tafsiri zilizomo katika mabango hayo.
Hicho ndicho kilichotuchochea kufanya utafiti ulioibua makala hii.
Jumla ya mabango 30 yalikusanywa kwa njia ya kupiga picha, kisha uchambuzi wa kimaudhui ulifanyika kuhusu mabango hayo.
Kwa hiyo, makala hii inabainisha makosa ya tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwenye mabango hayo.
Jumla ya mabango 30 yalitumika kama data.
Kwa kuongozwa na misingi ya Nadharia ya Usawe wa Kidhima, tulibainisha dosari mbalimbali za tafsiri zilizojidhihirisha katika mabango hayo.
Makosa yaliyobainishwa ni: makosa ya kisemantiki, makosa ya kimofolojia, makosa ya ki-tafsiri na makosa ya kisintaksia.
Makala imehitimishwa kwa kugusia vipengele vinavyoweza kuzingatiwa ili kupunguza dosari hizo.
Related Results
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili
Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulid...
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Utafiti huu unalenga kuchunguza kwa kina nafasi na athari za mwandishi anaposhiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutafsiri kazi yake ya kifasihi, kwa kuzingatia tamthilia mbili...
Mkakati wa Tafsiri Mkopo wa Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na Athari zake: Uchanganuzi wa Vidahizo Teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia
Mkakati wa Tafsiri Mkopo wa Istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na Athari zake: Uchanganuzi wa Vidahizo Teule vya Kamusi ya Biolojia, Fizikia na Kemia
Makala hii inachunguza mkakati wa tafsiri mkopo wa istilahi za Kiingereza katika Kiswahili na athari zake kwa kuangazia uga wa biolojia, fizikia na kemia kupitia vidahizo teule vya...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...