Javascript must be enabled to continue!
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
View through CrossRef
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo. Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikisha mazungumzo yao. Makala hii inachanganua mikakati ya upole inayotumiwa na wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma wanapoingiliana na abiria katika mji wa Matuu kwa kuzingatia lugha ya Kikamba. Mji wa Matuu upo katika kaunti ya Machakos, kaunti ndogo ya Yatta. Sampuli ya utafiti huu ilichaguliwa kimakusudi. Data ya utafiti huu ilikusanywa katika vituo vitatu vya magari ya uchukuzi katika mji wa Matuu vilivyoteuliwa kimakusudi. Mtafiti aliwahoji wahudumu ishirini na wawili na abiria kumi na tano. Mazungumzo kati ya wahudumu wa magari na abiria yalirekodiwa kwa kutumia kinasa sauti. Njia ya uchunguzi ilitumika kuchunguza mbinu ishara za kuwasiliana kama vile ishara za uso. Kauli zilizo na mikakati ya upole zilinakiliwa na kuwekwa kwenye makundi matano ya mikakati ya upole ili kuchanganuliwa. Makundi hayo ni: Mkakati wa kuwa kwenye rekodi, mkakati chanya wa upole, mkakati hasi wa upole, mkakati wa kuwa nje ya rekodi na mkakati wa kutosema chochote. Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1978, 1987). Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa wahudumu walitumia mikakati yote tano ya upole ili kulainisha mawasiliano kati yao na abiria. Mkakati chanya wa upole na mkakati hasi wa upole ndiyo iliyotumika kwa wingi na katika vituo vyote vitatu. Kupitia utafiti huu mtafiti anaamini kuwa washikadau katika sekta ya uchukuzi watapata maarifa kuhusu mbinu za kuwasiliana na abiria ili kutimiza malengo yao. Vile vile, kazi hii itasaidia kuboresha matumizi ya lugha kati ya wanajamii pamoja na kuongezea maarifa yaliyomo kuhusiana na taaluma ya isimujamii.
Editon Consortium Publishing
Title: Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Description:
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo.
Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikisha mazungumzo yao.
Makala hii inachanganua mikakati ya upole inayotumiwa na wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma wanapoingiliana na abiria katika mji wa Matuu kwa kuzingatia lugha ya Kikamba.
Mji wa Matuu upo katika kaunti ya Machakos, kaunti ndogo ya Yatta.
Sampuli ya utafiti huu ilichaguliwa kimakusudi.
Data ya utafiti huu ilikusanywa katika vituo vitatu vya magari ya uchukuzi katika mji wa Matuu vilivyoteuliwa kimakusudi.
Mtafiti aliwahoji wahudumu ishirini na wawili na abiria kumi na tano.
Mazungumzo kati ya wahudumu wa magari na abiria yalirekodiwa kwa kutumia kinasa sauti.
Njia ya uchunguzi ilitumika kuchunguza mbinu ishara za kuwasiliana kama vile ishara za uso.
Kauli zilizo na mikakati ya upole zilinakiliwa na kuwekwa kwenye makundi matano ya mikakati ya upole ili kuchanganuliwa.
Makundi hayo ni: Mkakati wa kuwa kwenye rekodi, mkakati chanya wa upole, mkakati hasi wa upole, mkakati wa kuwa nje ya rekodi na mkakati wa kutosema chochote.
Utafiti huu uliongozwa na mihimili ya Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1978, 1987).
Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa wahudumu walitumia mikakati yote tano ya upole ili kulainisha mawasiliano kati yao na abiria.
Mkakati chanya wa upole na mkakati hasi wa upole ndiyo iliyotumika kwa wingi na katika vituo vyote vitatu.
Kupitia utafiti huu mtafiti anaamini kuwa washikadau katika sekta ya uchukuzi watapata maarifa kuhusu mbinu za kuwasiliana na abiria ili kutimiza malengo yao.
Vile vile, kazi hii itasaidia kuboresha matumizi ya lugha kati ya wanajamii pamoja na kuongezea maarifa yaliyomo kuhusiana na taaluma ya isimujamii.
Related Results
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Ikisiri
Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...

