Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi

View through CrossRef
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jamii nyingi za Kiafrika humfungamanisha na jinsia ya kiume au kike kama ilivyo katika tamthilia ya Bembea ya Maisha iliyoandikwa na Timothy Arege mwaka wa 2020. Malengo ya Makala haya ni kutathmini jinsi masuala haya ya kijinsia yalivyo shughulikiwa na mwandishi huyu katika tamthilia hii. Nadharia itakayotumiwa kuendeleza kazi hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Chioma (1980) na kuendelezwa na watafiti wengine kama Ogundipe (1994), Wamitila (2003), Nnaemeka (2003) miongoni mwa wengine. Nadharia hii inalenga kutoa mwelekeo wa jinsi ya kumnasua mwanamke katika nafasi finyu aliyopewa katika jamii na nyanja tofauti. Data iliyotumika kuendeleza utafiti huu ilitoka maktabani kwa kusoma makala, vitabu, majarida na mambo mengine katika mtandao yanayohusiana na mada hii. Data inayohusiana na jinsia ya wahusika ilitoka katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.  Tamthilia ya Bembea ya Maisha iliteuliwa kimaksudi kwani mwandishi amewapa nafasi tosha wahusika wa jinsia ya kike na kiume. Wahusika hawa pia ni wa miaka tofauti kuanzia watoto hadi watu wazima. Mtafiti alisoma tamthilia husika na kuchambua wahusika kwa undani ili kupata data. Data iliyohitajika ilikusanywa na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na jedwali. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa, licha ya juhudi nyingi zilizofanywa ili kumpa mwanamke nafasi katika jamii, bado kuna baadhi ya waandishi ambao wamempa nafasi finyu au ya chini katika kazi zao za fasihi. Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua tamthilia ya Bembea ya Maisha. Data iliteuliwa kimakusudi. Mtafiti alizingatia nidhamu katika utafiti huu. Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa waandishi wa kazi za kifasihi ambao wanadhamiria kuandika kwani watajua namna ya kumsawiri mwanamke kama kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii. Aidha, wasomi wa fasihi za Kiafrika watapa taswira ya nafasi za kila jinsia katika jamii za Kiafrika
East African Nature and Science Organization
Title: Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Description:
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke.
Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili.
Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jamii nyingi za Kiafrika humfungamanisha na jinsia ya kiume au kike kama ilivyo katika tamthilia ya Bembea ya Maisha iliyoandikwa na Timothy Arege mwaka wa 2020.
Malengo ya Makala haya ni kutathmini jinsi masuala haya ya kijinsia yalivyo shughulikiwa na mwandishi huyu katika tamthilia hii.
Nadharia itakayotumiwa kuendeleza kazi hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika iliyoasisiwa na Chioma (1980) na kuendelezwa na watafiti wengine kama Ogundipe (1994), Wamitila (2003), Nnaemeka (2003) miongoni mwa wengine.
Nadharia hii inalenga kutoa mwelekeo wa jinsi ya kumnasua mwanamke katika nafasi finyu aliyopewa katika jamii na nyanja tofauti.
Data iliyotumika kuendeleza utafiti huu ilitoka maktabani kwa kusoma makala, vitabu, majarida na mambo mengine katika mtandao yanayohusiana na mada hii.
Data inayohusiana na jinsia ya wahusika ilitoka katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.
 Tamthilia ya Bembea ya Maisha iliteuliwa kimaksudi kwani mwandishi amewapa nafasi tosha wahusika wa jinsia ya kike na kiume.
Wahusika hawa pia ni wa miaka tofauti kuanzia watoto hadi watu wazima.
Mtafiti alisoma tamthilia husika na kuchambua wahusika kwa undani ili kupata data.
Data iliyohitajika ilikusanywa na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo na jedwali.
Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa, licha ya juhudi nyingi zilizofanywa ili kumpa mwanamke nafasi katika jamii, bado kuna baadhi ya waandishi ambao wamempa nafasi finyu au ya chini katika kazi zao za fasihi.
Usampulishaji dhamirifu ulitumika kuteua tamthilia ya Bembea ya Maisha.
Data iliteuliwa kimakusudi.
Mtafiti alizingatia nidhamu katika utafiti huu.
Utafiti huu utakuwa wa manufaa kwa waandishi wa kazi za kifasihi ambao wanadhamiria kuandika kwani watajua namna ya kumsawiri mwanamke kama kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii.
Aidha, wasomi wa fasihi za Kiafrika watapa taswira ya nafasi za kila jinsia katika jamii za Kiafrika.

Related Results

Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Ufanano wa Mtoto wa Laana Kumuua Babaye katika Nyakiiru Kibi na Mfalme Edipode: Dhihiriko la Umageuko au Msambao?
Ufanano wa Mtoto wa Laana Kumuua Babaye katika Nyakiiru Kibi na Mfalme Edipode: Dhihiriko la Umageuko au Msambao?
Ikisiri Kisa kinachoelezwa katika simulizi ya Edipode katika tamthilia ya Mfalme Edipode (Sofokile, 1971) kinafanana kwa karibu sana na kisa kinachosimuliwa katika Utenzi wa Nyakii...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Ushairi wa Simu Tamba wa Waswahili wa Pwani ya Kenya
Ushairi wa Simu Tamba wa Waswahili wa Pwani ya Kenya
Katika makala hii tunajadili jinsi simu tamba inavyotumika kama nyenzo katika uandishi, ukuzaji na usambazaji wa ushairi miongoni mwa Waswahili wa Pwani ya Kenya na hatimaye watu w...
Uchunguzi wa Mtagusano baina ya Hisia na Motifu: Mifano kutoka Tamthilia ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Uchunguzi wa Mtagusano baina ya Hisia na Motifu: Mifano kutoka Tamthilia ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
Motifu ni miongoni mwa vipengele vilivyochunguzwa kwenye matini za kifasihi andishi kwa mielekeo mbalimbali kama vile kuitumia kama nadharia ya uchambuzi na kama dhana ya uchambuzi...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...

Back to Top