Javascript must be enabled to continue!
Ufanano wa Mtoto wa Laana Kumuua Babaye katika Nyakiiru Kibi na Mfalme Edipode: Dhihiriko la Umageuko au Msambao?
View through CrossRef
Ikisiri
Kisa kinachoelezwa katika simulizi ya Edipode katika tamthilia ya Mfalme Edipode (Sofokile, 1971) kinafanana kwa karibu sana na kisa kinachosimuliwa katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi (Mulokozi, 1998). Sababu kubwa zilizochangia kufanana kwa simulizi hizi mbili zinaweza kuelezwa kwa kuzingatia misingi ya kinadharia, hususan Nadharia ya Mageuko na Nadharia ya Msambao. Wakati Nadharia ya Mageuko ikidai kuwa simulizi yoyote ile ni matokeo ya mabadiliko ya ndani ya jamii yanayochagizwa na mazingira, Nadharia ya Msambao inasisitiza kuwa simulizi huenea kutoka sehemu moja hadi nyingine; kamwe haiwezekani simulizi mbili zinazofanana kuibuka katika jamii mbili ambazo hazijawahi kukutana. Makala hii imechunguza sababu za kufanana kwa visa katika simulizi teule kwa kutumia misingi ya nadharia hizo mbili. Kwa kuzingatia hoja mbalimbali, imehitimishwa kuwa simulizi ya Nyakiiru Kibi, pamoja na kutungwa takribani karne 24 baada ya ile ya Edipode, si kiatani cha Edipode. Simulizi hii imechimbuka katika eneo la Maziwa Makuu na inaonekana ni tukio linalofungamana na historia ya jamii husika huku ikijumuisha visakale hapa na pale.
Title: Ufanano wa Mtoto wa Laana Kumuua Babaye katika Nyakiiru Kibi na Mfalme Edipode: Dhihiriko la Umageuko au Msambao?
Description:
Ikisiri
Kisa kinachoelezwa katika simulizi ya Edipode katika tamthilia ya Mfalme Edipode (Sofokile, 1971) kinafanana kwa karibu sana na kisa kinachosimuliwa katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi (Mulokozi, 1998).
Sababu kubwa zilizochangia kufanana kwa simulizi hizi mbili zinaweza kuelezwa kwa kuzingatia misingi ya kinadharia, hususan Nadharia ya Mageuko na Nadharia ya Msambao.
Wakati Nadharia ya Mageuko ikidai kuwa simulizi yoyote ile ni matokeo ya mabadiliko ya ndani ya jamii yanayochagizwa na mazingira, Nadharia ya Msambao inasisitiza kuwa simulizi huenea kutoka sehemu moja hadi nyingine; kamwe haiwezekani simulizi mbili zinazofanana kuibuka katika jamii mbili ambazo hazijawahi kukutana.
Makala hii imechunguza sababu za kufanana kwa visa katika simulizi teule kwa kutumia misingi ya nadharia hizo mbili.
Kwa kuzingatia hoja mbalimbali, imehitimishwa kuwa simulizi ya Nyakiiru Kibi, pamoja na kutungwa takribani karne 24 baada ya ile ya Edipode, si kiatani cha Edipode.
Simulizi hii imechimbuka katika eneo la Maziwa Makuu na inaonekana ni tukio linalofungamana na historia ya jamii husika huku ikijumuisha visakale hapa na pale.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Ruwaza za Toni katika Vitenzi Visoukomo Changamani vya Kirombo
Makala haya yanahusu uchanganuzi wa ruwaza za Toni katika Vitenzi visoukomo changamani vya Kirombo. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza ruwaza ya ujitokezaji wa toni katika vite...