Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ushairi wa Simu Tamba wa Waswahili wa Pwani ya Kenya

View through CrossRef
Katika makala hii tunajadili jinsi simu tamba inavyotumika kama nyenzo katika uandishi, ukuzaji na usambazaji wa ushairi miongoni mwa Waswahili wa Pwani ya Kenya na hatimaye watu wengine kote ulimwenguni. Ili kutimiza malengo haya tumetumia dhana ya utandawazi kama dhana changanuzi na vilevile Nadharia ya Kisosholojia ya Kiuhakiki lli kuchambua masuala ya kimaudhui ya ushairi wa simu tamba. Data ya utafiti huu imekusanywa kutokana na kutangamana na jumuiya ya Waswahili wa Pwani ya Kenya kupitia simu tamba. Mmoja wa waandishi wa kazi hii pia ni Mswahili wa Pwani ya Kenya na mshiriki katika mitagusano hii ya ushairi wa simu tamba. Katika kazi hii tumeangazia maudhui ya ushairi wa simu tamba miongoni mwa Waswahili wa Pwani ya Kenya na vilevile kuonesha baadhi ya mitindo inayopendelewa katika ushairi huu. Imebainika kuwa maudhui ya ushairi wa simu tamba katika eneo la Pwani ya Kenya yanahusu salamu za kutakiana heri siku ya Ijumaa na wakati wa mfungo wa Ramadhani. Masuala mengine ya kijamii yanayojitokeza ni yale yanayofungamana na ndoa, dini, uchumi na siasa. Imedhihirika pia kuwa mashairi ya simu tamba yanatungwa kwa kuzingatia kanuni za kijadi kama vile kuwa na urari wa vina, kupangilia shairi kwa kutumia beti, kuwa na mishororo iliyokadiriwa, na kuwa na urari wa vina na mizani. Mengi ya mashairi ya Waswahili wa Pwani ya Kenya ni ya muundo wa tathlitha na tarbia. Hata hivyo, kuna changamoto za kutunga na kuuendeleza ushairi wa Kiswahili kwa njia ya simu tamba kama vile ugumu wa kupangilia mishororo na hata vipande vya mashairi kwa namna inayofungamana na arudhi.
Title: Ushairi wa Simu Tamba wa Waswahili wa Pwani ya Kenya
Description:
Katika makala hii tunajadili jinsi simu tamba inavyotumika kama nyenzo katika uandishi, ukuzaji na usambazaji wa ushairi miongoni mwa Waswahili wa Pwani ya Kenya na hatimaye watu wengine kote ulimwenguni.
Ili kutimiza malengo haya tumetumia dhana ya utandawazi kama dhana changanuzi na vilevile Nadharia ya Kisosholojia ya Kiuhakiki lli kuchambua masuala ya kimaudhui ya ushairi wa simu tamba.
Data ya utafiti huu imekusanywa kutokana na kutangamana na jumuiya ya Waswahili wa Pwani ya Kenya kupitia simu tamba.
Mmoja wa waandishi wa kazi hii pia ni Mswahili wa Pwani ya Kenya na mshiriki katika mitagusano hii ya ushairi wa simu tamba.
Katika kazi hii tumeangazia maudhui ya ushairi wa simu tamba miongoni mwa Waswahili wa Pwani ya Kenya na vilevile kuonesha baadhi ya mitindo inayopendelewa katika ushairi huu.
Imebainika kuwa maudhui ya ushairi wa simu tamba katika eneo la Pwani ya Kenya yanahusu salamu za kutakiana heri siku ya Ijumaa na wakati wa mfungo wa Ramadhani.
Masuala mengine ya kijamii yanayojitokeza ni yale yanayofungamana na ndoa, dini, uchumi na siasa.
Imedhihirika pia kuwa mashairi ya simu tamba yanatungwa kwa kuzingatia kanuni za kijadi kama vile kuwa na urari wa vina, kupangilia shairi kwa kutumia beti, kuwa na mishororo iliyokadiriwa, na kuwa na urari wa vina na mizani.
Mengi ya mashairi ya Waswahili wa Pwani ya Kenya ni ya muundo wa tathlitha na tarbia.
Hata hivyo, kuna changamoto za kutunga na kuuendeleza ushairi wa Kiswahili kwa njia ya simu tamba kama vile ugumu wa kupangilia mishororo na hata vipande vya mashairi kwa namna inayofungamana na arudhi.

Related Results

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...
Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”
Uathirianomatini wa Kimtindo katika Ushairi wa Kiswahili: Mfano wa “Utenzi wa Hati” na “Utenzi wa Mwanakupona”
Bakhtin (1981) anaeleza kwamba matini za kifasihi huathiriana na kuhusiana. Kila matini ya kifasihi ina sauti zinazoingiliana na kuhusiana na matini nyingine zilizopo, zilizopita a...
Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
Sifa za Kimuundo Katika Diwani Huru ya Rangi ya Anga
Makala hii inalenga kuchambua na kutathmini sifa za kimuundo katika diwani huru ya Rangi ya Anga. Sifa za kimuundo ni muhimu katika kuudhibiti usomaji wa mashairi teule na kumwelek...
Digital Entrepreneurship and Performance of the Insurance Industry Sector in Kenya
Digital Entrepreneurship and Performance of the Insurance Industry Sector in Kenya
The insurance industry in Kenya has become very competitive due to the shrinking demand of noncompulsory insurance products and negative perception by the general public. To ensure...
Mafumbo ya mwanamke katika mashairi teule ya Muyaka
Mafumbo ya mwanamke katika mashairi teule ya Muyaka
Ikisiri Azma kuu ya makala hii ni kuchanganua mafumbo ya mwanamke wa Kiswahili wa karne ya kumi na tisa katika ushairi wa Kiswahili wa kipindi hicho. Kwa kutumia mashairi teule ya ...
Resistance levels of cassava landraces to CMD, CBSD and vector whiteflies in Malawi
Resistance levels of cassava landraces to CMD, CBSD and vector whiteflies in Malawi
Abstract Cassava mosaic disease (CMD) and cassava brown streak disease (CBSD) have been two major threats to cassava production in eastern and southern Africa. This study w...

Back to Top