Javascript must be enabled to continue!
Tafsiri ya Lugha ya Ishara katika Wema Hawajazaliwa: Mtazamo wa Ulinganifu wa Kimawasiliano
View through CrossRef
Tafsiri ni taaluma kongwe ambayo imekuwa ikifanyika katika nyuga mbalimbali kama vile sheria, utabibu na lugha. Tafiti nyingi zimekitwa katika matatizo ya tafsiri kwa ujumla. Wataalamu wa tafsiri, hususani za kifasihi kama vile Mkinga (2005), Malangwa (2010) na Mekacha (2013), wametafiti kuhusu mbinu na matatizo ya kutafsiri matini za kifasihi. Data za makala hii zimetokana na mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili. Wafasiri tofauti wametafsiri kazi za kifasihi kwa kuzingatia usanaa uliomo kwenye kazi husika. Makala hii inamulika tafsiri ya lugha ya ishara katika Wema Hawajazaliwa kwa kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa kimawasiliano. Wema Hawajazaliwa ni riwaya iliyotafsiriwa na Abdilatif Abdallah kutoka katika riwaya ya The Beautyful Ones are not Yet Born ya Ayi Kwei Armah. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano iliyoasisiwa na Nida (1964). Pamoja na wataalamu wengi kutafiti kuhusu matatizo ya tafsiri, bado tafsiri ya kifasihi haijafanyiwa tafiti za kutosha hususani katika lugha ya Kiswahili. Makala hii imebaini kuwa, mfasiri huzingatia lugha ya ishara katika tafsiri ya matukio mbalimbali ya kiishara.
Title: Tafsiri ya Lugha ya Ishara katika Wema Hawajazaliwa: Mtazamo wa Ulinganifu wa Kimawasiliano
Description:
Tafsiri ni taaluma kongwe ambayo imekuwa ikifanyika katika nyuga mbalimbali kama vile sheria, utabibu na lugha.
Tafiti nyingi zimekitwa katika matatizo ya tafsiri kwa ujumla.
Wataalamu wa tafsiri, hususani za kifasihi kama vile Mkinga (2005), Malangwa (2010) na Mekacha (2013), wametafiti kuhusu mbinu na matatizo ya kutafsiri matini za kifasihi.
Data za makala hii zimetokana na mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili.
Wafasiri tofauti wametafsiri kazi za kifasihi kwa kuzingatia usanaa uliomo kwenye kazi husika.
Makala hii inamulika tafsiri ya lugha ya ishara katika Wema Hawajazaliwa kwa kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa kimawasiliano.
Wema Hawajazaliwa ni riwaya iliyotafsiriwa na Abdilatif Abdallah kutoka katika riwaya ya The Beautyful Ones are not Yet Born ya Ayi Kwei Armah.
Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano iliyoasisiwa na Nida (1964).
Pamoja na wataalamu wengi kutafiti kuhusu matatizo ya tafsiri, bado tafsiri ya kifasihi haijafanyiwa tafiti za kutosha hususani katika lugha ya Kiswahili.
Makala hii imebaini kuwa, mfasiri huzingatia lugha ya ishara katika tafsiri ya matukio mbalimbali ya kiishara.
Related Results
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Mtunzi kama Mtafsiri Anayeingilia Kati ya Tafsiri: Kifo Kisimani (1999) na Natala (2005)
Utafiti huu unalenga kuchunguza kwa kina nafasi na athari za mwandishi anaposhiriki moja kwa moja katika mchakato wa kutafsiri kazi yake ya kifasihi, kwa kuzingatia tamthilia mbili...
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Uamilifu wa Kiswahili na Kibukusu katika Mawanda ya Kimatumizi kwenye Kaunti ya Bungoma
Lugha ni chombo maalum katika ustawishaji na uimarishaji wa rasilimali za mwanadamu. Pia, ni wenzo unaohimili sera ambazo hulenga katika kutimiza matarajio ya kitaifa katika nchi y...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Utangamano baina ya Lugha ya Kiswahili na Lugha ya Kinyambo Kimofolojia: Uchambuzi wa Maeneo Mahususi
Lengo la makala haya ni kuonesha utangamano wa lugha ya Kiswahili na lugha ya Kinyambo. Utangamano wa lugha hizo umeoneshwa katika baadhi ya vipengele vya kimofolojia ambavyo ni mb...