Javascript must be enabled to continue!
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
View through CrossRef
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, utafiti huu umechunguza changamoto au ugumu wanaokumbana nao wanukuzi wa maandishi haya na athari yake kwa wanafunzi wasioona katika elimu. Utafiti wa nyanjani ndio uliofaa kazi hii, nazo mbinu za kukusanya data zilizozofaa ni hojaji na mahojiano. Wanafunzi walipewa kazi ya kuandika insha zilizopewa wanukuzi walizozinukuu ili kuchanganuliwa. Uchunguzi huu ulikusudiwa kufanywa katika vyuo vya elimu kama vile Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Maseno, Taasisi ya Elimu ya Machakos, Taasisi ya Wasioona ya Kenya na Taasisi ya Elimu ya Kagumo kwa sababu vyuo hivi ndivyo vilivyo na wahadhiri wengi wasiojua kusoma breili na mara nyingi husaidiwa na wanukuzi kunukuu kazi za breili katika maandishi ya kawaida ili wakapate kusoma na kuelewa. Kutokana na utafiti huu ni wazi kuwa tafsiri ya breili ya Kiswahili hadi maandishi ya kawaida imepungukiwa katika kuwasilisha maana iliyokusudiwa kwa sababu ya ukosefu wa breili sanifu ya Kiswahili, kuwepo kwa changamoto zilizofafanuliwa katika tasnifu hii na ukosefu wa umilisi katika breili ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na wanukuzi huathiri pakubwa tafsiri ya maandishi haya. Utafiti huu utawanufaisha wanaotumia breili, walimu wao na wanukuzi wa maandishi haya ya breili
East African Nature and Science Organization
Title: Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Description:
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa.
Katika kutimiza lengo hilo, utafiti huu umechunguza changamoto au ugumu wanaokumbana nao wanukuzi wa maandishi haya na athari yake kwa wanafunzi wasioona katika elimu.
Utafiti wa nyanjani ndio uliofaa kazi hii, nazo mbinu za kukusanya data zilizozofaa ni hojaji na mahojiano.
Wanafunzi walipewa kazi ya kuandika insha zilizopewa wanukuzi walizozinukuu ili kuchanganuliwa.
Uchunguzi huu ulikusudiwa kufanywa katika vyuo vya elimu kama vile Chuo Kikuu cha Kenyatta, Chuo Kikuu cha Maseno, Taasisi ya Elimu ya Machakos, Taasisi ya Wasioona ya Kenya na Taasisi ya Elimu ya Kagumo kwa sababu vyuo hivi ndivyo vilivyo na wahadhiri wengi wasiojua kusoma breili na mara nyingi husaidiwa na wanukuzi kunukuu kazi za breili katika maandishi ya kawaida ili wakapate kusoma na kuelewa.
Kutokana na utafiti huu ni wazi kuwa tafsiri ya breili ya Kiswahili hadi maandishi ya kawaida imepungukiwa katika kuwasilisha maana iliyokusudiwa kwa sababu ya ukosefu wa breili sanifu ya Kiswahili, kuwepo kwa changamoto zilizofafanuliwa katika tasnifu hii na ukosefu wa umilisi katika breili ya Kiswahili miongoni mwa wanafunzi na wanukuzi huathiri pakubwa tafsiri ya maandishi haya.
Utafiti huu utawanufaisha wanaotumia breili, walimu wao na wanukuzi wa maandishi haya ya breili.
Related Results
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...


