Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"

View through CrossRef
Kazi ya fasihi ikiwemo riwaya huundwa na fani na maudhui, ambavyo kwa pamoja ndivyo hutupatia kazi inayoitwa fasihi. Fani huundwa na vipengele kama vile wahusika, mtindo, mandhari, muundo na matumizi ya lugha. Vipengele hivi hutumiwa na waandishi kwa namna tofauti tofauti kulingana na ujuzi na welei wao. Kwa upande wa maudhui ni jumla ya mawazo makuu yanayoelezwa na mwandishi au msimulizi wa kazi ya fasihi na kutaka hadhira yake ipate . kazi huu ulikusudiwa kufanywa kwa nia ya kuchunguza dhamira mbalimbali ambazo zinawasilishwa na Mohamed Suleiman katika riwaya yake ya Kiu. Kupita riwaya hii tumeainisha na mbinu za kifani zilizotumiwa na mwandishi katika kuibua dhamira ndani ya riwaya hiyo. Kiu ni riwaya ya Kiswahili inayoelezea hadithi ya Bahati, kijana mwanamke aliyelelewa akaleleka na sasa anakutana na Idi, mwanaume laghai. Iddi hakawii kumzonga Bahati kwa kamba ya mapenzi ya uwongo. Bahati akiwa kalowa mapenzi hajijui hajitambui, anang’amua kuwa Iddi kwa kweli hampendi yeye, bali nafsi yake mwenyewe, na yeye Bahati ni chombo tu cha kutimiza shauku zake za kilimwengu. Kama ndege aliyenaswa katika ulimbo, jitihada zake za kujipatia nusura zinamletea angamio.
Title: Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"
Description:
Kazi ya fasihi ikiwemo riwaya huundwa na fani na maudhui, ambavyo kwa pamoja ndivyo hutupatia kazi inayoitwa fasihi.
Fani huundwa na vipengele kama vile wahusika, mtindo, mandhari, muundo na matumizi ya lugha.
Vipengele hivi hutumiwa na waandishi kwa namna tofauti tofauti kulingana na ujuzi na welei wao.
Kwa upande wa maudhui ni jumla ya mawazo makuu yanayoelezwa na mwandishi au msimulizi wa kazi ya fasihi na kutaka hadhira yake ipate .
kazi huu ulikusudiwa kufanywa kwa nia ya kuchunguza dhamira mbalimbali ambazo zinawasilishwa na Mohamed Suleiman katika riwaya yake ya Kiu.
Kupita riwaya hii tumeainisha na mbinu za kifani zilizotumiwa na mwandishi katika kuibua dhamira ndani ya riwaya hiyo.
Kiu ni riwaya ya Kiswahili inayoelezea hadithi ya Bahati, kijana mwanamke aliyelelewa akaleleka na sasa anakutana na Idi, mwanaume laghai.
Iddi hakawii kumzonga Bahati kwa kamba ya mapenzi ya uwongo.
Bahati akiwa kalowa mapenzi hajijui hajitambui, anang’amua kuwa Iddi kwa kweli hampendi yeye, bali nafsi yake mwenyewe, na yeye Bahati ni chombo tu cha kutimiza shauku zake za kilimwengu.
Kama ndege aliyenaswa katika ulimbo, jitihada zake za kujipatia nusura zinamletea angamio.

Related Results

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Nafasi ya Kiswahili katika Ujenzi wa Utamaduni wa Uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, Kenya
Swahili Lengo la makala haya ni kupambanua nafasi ya Kiswahili katika ujenzi wa utamaduni wa uongozi katika Shule ya Msingi ya Mungakha, Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya. Uongozi w...

Back to Top