Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Uamilifu wa Mofu {(-)i-} katika Kiswahili Kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

View through CrossRef
Makala hii inachunguza uamilifu wa mofu {(-)i-} katika Kiswahili kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Data zilizotumiwa zilikusanywa kutoka katika vipindi mbalimbali vya lugha ya Kiswahili vya redio zinazosikika mjini Bujumbura nchini Burundi, na Uvira, Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Redio husika ni Redio-Televisheni ya Taifa ya Burundi (Radio-Télévision Nationale du Burundi, RTNB), Redio-Televisheni Isanganiro (Radio Télévision Isanganiro), Redio Bonesha FM, Redio Maendeleo ya Bukavu Kusini na Redio ya Umma ya Kivu Kusini (Radio Communautaire Thématique). Mbinu ya usikilizaji makini katika kusikiliza redio na uandishi zilitumiwa katika kukusanya data ambazo zilichanganuliwa kwa njia ya uchambuzi wa maumbo ya maneno. Nadharia ya Mofolojia ya Muunganiko wa Mofu ya Fradin (2003) na Nadharia ya Umiliki na Ufungati ya Chomsky (1981) ndizo zilizoongoza utafiti huu. Uchunguzi wa data ulidhihirisha mambo kadhaa. Kwanza, mofu {(-)i-} ambayo kwa kawaida wingi wake ni {zi-} huweza kuwakilisha ngeli zingine zozote katika neno husika na kuwa kibadala chake. Pili, matumizi ya mofu {(-)i-} hayazingatii idadi, hali ambayo huifanya kuashiria ama umoja au wingi. Tatu, huwa na uamilifu wa kiambishi cha upatanisho wa kisarufi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, ingawa mofu {(-)i-} ina uamilifu wa kimofosintaksia, hudhihirisha kutopatana kwa vipashio vya tungo katika Kiswahili kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Title: Uamilifu wa Mofu {(-)i-} katika Kiswahili Kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Description:
Makala hii inachunguza uamilifu wa mofu {(-)i-} katika Kiswahili kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Data zilizotumiwa zilikusanywa kutoka katika vipindi mbalimbali vya lugha ya Kiswahili vya redio zinazosikika mjini Bujumbura nchini Burundi, na Uvira, Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Redio husika ni Redio-Televisheni ya Taifa ya Burundi (Radio-Télévision Nationale du Burundi, RTNB), Redio-Televisheni Isanganiro (Radio Télévision Isanganiro), Redio Bonesha FM, Redio Maendeleo ya Bukavu Kusini na Redio ya Umma ya Kivu Kusini (Radio Communautaire Thématique).
Mbinu ya usikilizaji makini katika kusikiliza redio na uandishi zilitumiwa katika kukusanya data ambazo zilichanganuliwa kwa njia ya uchambuzi wa maumbo ya maneno.
Nadharia ya Mofolojia ya Muunganiko wa Mofu ya Fradin (2003) na Nadharia ya Umiliki na Ufungati ya Chomsky (1981) ndizo zilizoongoza utafiti huu.
Uchunguzi wa data ulidhihirisha mambo kadhaa.
Kwanza, mofu {(-)i-} ambayo kwa kawaida wingi wake ni {zi-} huweza kuwakilisha ngeli zingine zozote katika neno husika na kuwa kibadala chake.
Pili, matumizi ya mofu {(-)i-} hayazingatii idadi, hali ambayo huifanya kuashiria ama umoja au wingi.
Tatu, huwa na uamilifu wa kiambishi cha upatanisho wa kisarufi.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu, ingawa mofu {(-)i-} ina uamilifu wa kimofosintaksia, hudhihirisha kutopatana kwa vipashio vya tungo katika Kiswahili kinachozungumzwa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Related Results

Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Matumizi ya Kiswahili katika Ujumuishaji wa Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Nchini Tanzania
Makala haya yanaeleza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ujumuishaji wa kidemokrasia nchini Tanzania kwa kuzingatia matumizi ya lugha hiyo kwenye michakato ya uchaguzi. Lengo la...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Athari za Mtaala wa Umilisi katika Ukuzaji wa Umahiri wa Kuzungumza Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda
Umahiri wa kuzungumza lugha ni miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa kutoka kwa mtu yeyote anayejifunza lugha ya kigeni au lugha ya pili. Mathalani nchini Uganda imebainika kuwa kiwa...
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Ubainishaji wa Vipengele vya Ujumi wa Kiafrika na Athari yake katika Ushairi wa Kiswahili: Uchunguzi wa Ushairi wa Bongo Fleva
Makala haya yalichunguza ujitokezaji wa ujumi wa Kiafrika katika ushairi wa Kiswahili wa Bongo Fleva pamoja na athari yake katika ushairi huo. Tafiti kuhusu vipengele vya ujumi wa ...

Back to Top