Javascript must be enabled to continue!
Nafasi ya Tashbihi katika Kufanikisha Maudhui katika Fasihi ya Watoto
View through CrossRef
Makala haya yalichunguza jinsi wasanii wa vitabu vya fasihi ya watoto wamefuma tashbihi katika kazi zao ili kueleza maudhui yanayowalenga watoto kwa kuongozwa na nadharia ya umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916). Kupitia kwa njia ya kiupekuzi na uchanganuzi matini, vitabu vya Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwana viliteuliwa kimakusudi, vikasomwa na kuchanganuliwa. Tashbihi mbalimbali na maudhui ya familia, elimu, nidhamu, bidii, ugonjwa na kifo yalitambuliwa na kujadiliwa kwa undani. Uhusiano kati ya tashbihi na maudhui hayo ulidhihirishwa. Matokeo ya jinsi tashbihi zinavyofanikisha kueleza maudhui yaliwasilishwa kithamano. Utafiti huu umeonyesha tashbihi na maudhui katika kazi tulizohakiki na pia unachochea washikadau katika uwanda wa fasihi ya watoto kuhakiki kazi za watoto kabla kuwateulia kuzisoma.
East African Nature and Science Organization
Title: Nafasi ya Tashbihi katika Kufanikisha Maudhui katika Fasihi ya Watoto
Description:
Makala haya yalichunguza jinsi wasanii wa vitabu vya fasihi ya watoto wamefuma tashbihi katika kazi zao ili kueleza maudhui yanayowalenga watoto kwa kuongozwa na nadharia ya umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1916).
Kupitia kwa njia ya kiupekuzi na uchanganuzi matini, vitabu vya Kisasi Hapana, Nimefufuka, Sitaki Iwe Siri, na Wema wa Mwana viliteuliwa kimakusudi, vikasomwa na kuchanganuliwa.
Tashbihi mbalimbali na maudhui ya familia, elimu, nidhamu, bidii, ugonjwa na kifo yalitambuliwa na kujadiliwa kwa undani.
Uhusiano kati ya tashbihi na maudhui hayo ulidhihirishwa.
Matokeo ya jinsi tashbihi zinavyofanikisha kueleza maudhui yaliwasilishwa kithamano.
Utafiti huu umeonyesha tashbihi na maudhui katika kazi tulizohakiki na pia unachochea washikadau katika uwanda wa fasihi ya watoto kuhakiki kazi za watoto kabla kuwateulia kuzisoma.
Related Results
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Maudhui ya Malezi ya Watoto katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Tumaini na Mshale wa Matumaini
Kila mtoto huhitaji malezi thabiti katika maisha ili kumkuza katika uadilifu wa siku za baadaye. Utafiti huu ulishughulikia maudhui ya malezi ya watoto kwa kuegemea fasihi ya watot...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha za Kiafrika Kuelekeza Wasichana Katika Masuala ya Ndoa: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi ...