Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu

View through CrossRef
Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria. Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano. Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi. Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi. Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria. Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria. Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki. Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani. Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano. Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo. Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini. Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu. Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria. Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.
Title: Nafasi Ya Fasihi Simulizi Katika Kuwasilisha Ujumbe Kisheria: Mfano wa Uendeshaji Kesi Za Kitamaduni Miongoni Mwa Babukusu
Description:
Utafiti uliazimia kubainisha nafasi ya Fasihi Simulizi katika kuwasilisha ujumbe kisheria.
Ulionyesha namna vipengele bainifu vya Fasihi Simulizi vinaweza kutumika kuwasilisha ujumbe kisheria.
Ulifanya hivyo kwa kuegemea uendeshaji wa kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu.
Ili kuafikia lengo hili utafiti ulitumia mbinu ya kithamano.
Idadi lengwa ya utafiti ilikuwa jumla ya kesi za kitamaduni tulizohudhuria na kuzirekodi.
Utafiti ulijumuisha mbinu ya uteuzi wa sampuli kimaksudi.
Uteuzi wa sampuli kimaksudi ulitumiwa kuchagua Chifu, naibu wa Chifu, mwenyekiti wa baraza la wazee na makala maalum yaliyoandikwa kuhusu Fasihi Simulizi na Sheria.
Nao uteuzi wa sampuli kinasibu ulitumiwa kuteua mabaraza ya wazee na ya Chifu tuliohudhuria.
Waaidha, uchunguzi ulihusisha mbinu za uchambuzi wa yaliyomo, usaili na uchunzaji-shiriki.
Njia hizi zilitumika kukusanya data nyanjani na maktabani.
Matokeo ya utafiti yalichanganuliwa kithamano.
Hii ni mbinu ya kuchanganua data ambayo mtafiti anaeleza na kufafanua matokeo ya utafiti wake kimaelezo.
Uchunguzi huu vilevile uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini.
Kwa mujibu wa kesi tulizohudhuria, utafiti ulibaini kuwa kuna vipengele vya Fasihi Simulizi ambavyo vinaoana na hali ilivyo katika taaluma ya Sheria wakati wa uendeshaj kesi kitamaduni miongoni mwa jamii ya Babukusu.
Kwa hivyo ni muhali kusema kuwa matini za Kifasihi Simulizi huwa zinachota, kunukuu, kugeuza, kuiga kwa namna ya kufumba, kubeza au kurejelea kwa njia moja ama nyingine matini za Kisheria.
Hali kadhalika tanzu zenyewe za Fasihi Simulizi zinaingiliana na kuchangiana katika kutimiza mahitaji ya jamii kupitia shughuli mbalimbali.

Related Results

Microwave Ablation with or Without Chemotherapy in Management of Non-Small Cell Lung Cancer: A Systematic Review
Microwave Ablation with or Without Chemotherapy in Management of Non-Small Cell Lung Cancer: A Systematic Review
Abstract Introduction  Microwave ablation (MWA) has emerged as a minimally invasive treatment for patients with inoperable non-small cell lung cancer (NSCLC). However, whether it i...
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Vipengele Vya Fasihi Vinavyojenga Taswira Ya Mwanamke Katikavitabu Teule Vya Biblia Takatifu
Lugha ni chombo cha kipekee kinachofinyangwa kuwasilisha taswira ya masuala changamano katika jamii. Matokeo haya ya lugha ni fasihi, ambayo ni kioo cha jamii. Biblia Takatifu ni k...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Umuhimu wa mafumbo yanayotumika katika miktadha ya wosia wa babu kwa wavulana miongoni mwa Wabukusu wa Kenya.
Umuhimu wa mafumbo yanayotumika katika miktadha ya wosia wa babu kwa wavulana miongoni mwa Wabukusu wa Kenya.
IKISIRI Utafiti huu ulihakiki umuhimu wa mafumbo yanayotumiwa katika miktadha ya wosia wa babu kwa wavulana miongoni mwa Wabukusu wa Kenya. Mafumbo ni kipera cha semi katika ...
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Ujitokezaji wa Viarudhi vya Kifonolojia katika Kihaya: Uchunguzi Kifani wa Toni katika Lahaja ya Kihamba
Fonolojia ni taaluma iliyosheheni viarudhi au vipambasauti kama ambavyo wataalamu wengine huviita. Miongoni mwake ni toni, lafudhi, mkazo, nguvumsikiko, usilabi, kiimbo, unguvunguv...
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Maudhui katika Nyimbo Teule Kwenye Kipindi cha Rauka
Utafiti huu unahusu maudhui katika nyimbo teule kwenye vyombo vya habari, mfano ni nyimbo katika kipindi cha Rauka katika runinga ya Citizen. Utafiti ulichochewa na haja ya kutaka ...
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Matumizi ya Kiswahili katika Mawasiliano na Uongozi wa Kidini katika Shule za Upili Nchini Kenya: Mfano wa Shule ya Wasichana ya Itigo
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya Kiswahili katika mawasiliano na uongozi wa kidini katika shule ya wasichana ya Itigo. Ulilenga kubaini jinsi lugha ya Kiswahili hutumika katika ...

Back to Top