Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi

View through CrossRef
Mfuatano wa irabu katika lugha nyingi za Kibantu haupendelewi katika mazungumzo. Huepukwa kwa kutumia ukarabati wa namna mbalimbali. Kwa hiyo, makala hii inahusu ukarabati unaofanyika ili kuepukana na kutumia irabu zinazofuatana katika mpaka wa kisintaksia, yaani baina ya maneno yanayofuatana katika Gᴉrᴉmi (F32). Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia imetumika kuchambua na kujadili data za makala hii. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni mbili: mbinu ya uhakiki wa kisarufi na ya usaili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, katika Gᴉrᴉmi, ukarabati wa mfuatano wa irabu baina ya neno na neno hufanywa kwa kutumia michakato mitatu ya kifonolojia ambayo ni mvutano wa irabu, udondoshaji wa irabu na uyeyushaji wa irabu. Ukarabati huo hufanyika kurahisisha matamshi na mazungumzo. Kufuatia matokeo haya, makala inapendekeza tafiti zaidi kufanyika ili kubaini jinsi mifanyiko ya kifonolojia inavyokarabati matamshi ya maneno yanayohusisha mfuatano wa irabu katika lugha zingine, hasa za Kibantu.
African Journals Online (AJOL)
Title: Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi
Description:
Mfuatano wa irabu katika lugha nyingi za Kibantu haupendelewi katika mazungumzo.
Huepukwa kwa kutumia ukarabati wa namna mbalimbali.
Kwa hiyo, makala hii inahusu ukarabati unaofanyika ili kuepukana na kutumia irabu zinazofuatana katika mpaka wa kisintaksia, yaani baina ya maneno yanayofuatana katika Gᴉrᴉmi (F32).
Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia imetumika kuchambua na kujadili data za makala hii.
Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni mbili: mbinu ya uhakiki wa kisarufi na ya usaili.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, katika Gᴉrᴉmi, ukarabati wa mfuatano wa irabu baina ya neno na neno hufanywa kwa kutumia michakato mitatu ya kifonolojia ambayo ni mvutano wa irabu, udondoshaji wa irabu na uyeyushaji wa irabu.
Ukarabati huo hufanyika kurahisisha matamshi na mazungumzo.
Kufuatia matokeo haya, makala inapendekeza tafiti zaidi kufanyika ili kubaini jinsi mifanyiko ya kifonolojia inavyokarabati matamshi ya maneno yanayohusisha mfuatano wa irabu katika lugha zingine, hasa za Kibantu.

Related Results

Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili
Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi. Ikiwa kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano ...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Ikisiri Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchu...

Back to Top