Javascript must be enabled to continue!
Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi
View through CrossRef
Watu wenye uwezo na mamlaka wanatumia madaraka yao kuwatawala wengine kwa vishawishianuwai. Asasi za kijamii kama vile ndoa, shule, vyuo, utamaduni na malezi zinaendelea kushuhudiautawala wa wenye uwezo juu ya wasio na uwezo. Licha ya ubayana wa hali hii katika jamii, watafiti na wahakiki wa tanzu za fasihi andishi hususan riwaya hawajaonyesha namna hejemonia
inajitokeza katika asasi za kijamii. Ingawa wahakiki wengi wa riwaya wameweza kuangazia masualaya kila nui kuhusu asasi za kijamii, suala la hejemonia katika taasisi hizo lilihitaji kumulikwa. Hivyo,utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ujitokezaji wa hejemonia katika safu ya hejemonia ya jamii kwa mujibu wa riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi.Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hejemonia ilioasisiwa na Antonio Gramsci katika makala
aliyoyaandika akiwa gerezani kati ya mwaka wa 1923 na 1936. Nadharia hii inaelezea udumishaji wauwezo na mamlaka ya tabaka moja kuu juu ya tabaka dogo kwa kutumia mikakati anuwai. Utafitihuu ulifanyiwa maktabani ambako utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kithamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Matokeo ya utafiti huu yatawafaa wahakiki na watafiti wa lugha na fasihi huku yakiweka wazi uwepo wa hejemonia katika asasi za jamii.
Editon Consortium Publishing
Title: Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi
Description:
Watu wenye uwezo na mamlaka wanatumia madaraka yao kuwatawala wengine kwa vishawishianuwai.
Asasi za kijamii kama vile ndoa, shule, vyuo, utamaduni na malezi zinaendelea kushuhudiautawala wa wenye uwezo juu ya wasio na uwezo.
Licha ya ubayana wa hali hii katika jamii, watafiti na wahakiki wa tanzu za fasihi andishi hususan riwaya hawajaonyesha namna hejemonia
inajitokeza katika asasi za kijamii.
Ingawa wahakiki wengi wa riwaya wameweza kuangazia masualaya kila nui kuhusu asasi za kijamii, suala la hejemonia katika taasisi hizo lilihitaji kumulikwa.
Hivyo,utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ujitokezaji wa hejemonia katika safu ya hejemonia ya jamii kwa mujibu wa riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi.
Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hejemonia ilioasisiwa na Antonio Gramsci katika makala
aliyoyaandika akiwa gerezani kati ya mwaka wa 1923 na 1936.
Nadharia hii inaelezea udumishaji wauwezo na mamlaka ya tabaka moja kuu juu ya tabaka dogo kwa kutumia mikakati anuwai.
Utafitihuu ulifanyiwa maktabani ambako utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kithamano ikitumika kuchanganua data hiyo.
Matokeo ya utafiti huu yatawafaa wahakiki na watafiti wa lugha na fasihi huku yakiweka wazi uwepo wa hejemonia katika asasi za jamii.
Related Results
Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi
Propaganda Kama Mkakati wa Kuhimili Hejemonia: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi
Makala hii imechunguza suala la propaganda kama mkakati wa kuhimili hejemonia katika riwaya teule za Kiswahili. Mtafiti amejadili namna propaganda inatumiwa kudumisha na kuimarisha...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano
Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi. Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho kinapa...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...

