Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya

View through CrossRef
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawasiliano rasmi, hasa ikilinganishwa na Kiingereza. Lengo la utafiti lilikuwa kubainisha mikakati ambayo Kiswahili kinatumia kukua na kufanikisha mawasiliano rasmi. Data ilikusanywa kutoka kwa maandishi mbalimbali na Kamusi Pevu ya Kiswahili (2016). Utafiti huu uliozaa makala haya ulionesha kwamba Kiswahili kinatumia mikakati ya urekebu wa kifonolojia na kisemantiki kupata msamiati na istilahi za kufanikisha mawasiliano. Utafiti unapendekeza kuundwa kwa chombo cha kitaifa kusimamia maendeleo ya msamiati wa Kiswahili na kupendekeza Kiswahili kiweze kutumika katika mawanda yote, yakiwemo rasmi, ili kiweze kufanikisha majukumu yake mapya. Aidha, makala haya yanapendekeza kuwa Kiswahili kinastahili kutumiwa katika mawanda yote ili kiweze kurekebu na kuyafanikisha majukumu yake mapya ya kimawasiliano kama lugha rasmi nchini Kenya
Title: Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Description:
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawasiliano rasmi, hasa ikilinganishwa na Kiingereza.
Lengo la utafiti lilikuwa kubainisha mikakati ambayo Kiswahili kinatumia kukua na kufanikisha mawasiliano rasmi.
Data ilikusanywa kutoka kwa maandishi mbalimbali na Kamusi Pevu ya Kiswahili (2016).
Utafiti huu uliozaa makala haya ulionesha kwamba Kiswahili kinatumia mikakati ya urekebu wa kifonolojia na kisemantiki kupata msamiati na istilahi za kufanikisha mawasiliano.
Utafiti unapendekeza kuundwa kwa chombo cha kitaifa kusimamia maendeleo ya msamiati wa Kiswahili na kupendekeza Kiswahili kiweze kutumika katika mawanda yote, yakiwemo rasmi, ili kiweze kufanikisha majukumu yake mapya.
Aidha, makala haya yanapendekeza kuwa Kiswahili kinastahili kutumiwa katika mawanda yote ili kiweze kurekebu na kuyafanikisha majukumu yake mapya ya kimawasiliano kama lugha rasmi nchini Kenya.

Related Results

Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Mikakati ya Upole Katika Mawasiliano ya Wahudumu wa Magari ya Uchukuzi na Abiria katika lugha ya Kikamba.
Upole ni hali ya msemaji kudhihirisha kuwa anajali hisia na mahitaji ya msikilizaji katika mazungumzo. Mikakati ya upole hutumiwa na washiriki wa mazungumzo kulainisha na kufanikis...
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Ikisiri Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...
The Englishization of Tanzanian Kiswahili
The Englishization of Tanzanian Kiswahili
ABSTRACT: The paper discusses the influence of English on Kiswahili, namely, the Englishization of Kiswahili on the basis of data extracted from various recent textbooks, pop stor...

Back to Top