Javascript must be enabled to continue!
Kuchanganua Aina za Mageuzi katika Maneno ya Sentensi Sahili ya Ekegusii.
View through CrossRef
Utafiti huu unachanganua aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo. Data ilikusanywa maktabani kutumia kifaa cha kudondoa data, kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii. Ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi, mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa. Mbinu za maelezo zilitumika katika uwasilishaji wa data. Mchakato hufanywa kwa kufuata kanuni mahsusi zinazoitwa kanuni geuzi. Ugeuzi unafuata utaratibu maalum, haufanywi kiholela. Katika ugeuzi wa maumbo kuna sharti la ukaribu ambapo hakuna kiambajengo kinaweza kuhamishwa zaidi ya fundo funge mbili kutokana na matokeo ya utafiti huu. Kanuni zingine za uhamisho ni kanuni ya ufungami ambapo muundo wa kijenzi kilichofundwa unahitaji uamuliwe na neno tawala linalofaa. Kuna vilele kanuni ya ulafi, kanuni teta na kanuni hamishe. Mwisho kuna kanuni muundo virai, kanuni geuzi na kanuni za mofofonemiki. Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu aina zingine za mageuzi kama vile, geuzi hamishi swalifu, geuzi hamishi la yambwa tendewa katika lugha hii na hata lugha nyinginezo ili kukuza uwanja wa kisintaksia. Kuna uhamisho unaotokea kwa lugha zingine na siyo katika Ekegusii. Hizi pia zinaweza kufanyiwa utafiti. Tafiti zaidi zinaweza kufanyiwa mada hii kwa kutumia nadharia zingine ili kueleza ikiwa kutakuwa na matokeo tofauti.
Title: Kuchanganua Aina za Mageuzi katika Maneno ya Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Description:
Utafiti huu unachanganua aina za mageuzi zinazojitokeza katika sentensi sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia za Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo.
Data ilikusanywa maktabani kutumia kifaa cha kudondoa data, kupitia kwa vitabu teule vya Ekegusii.
Ili kupata sentensi zilizodhihirisha mageuzi, mbinu ya usampulishaji kwa lengo maalum ilitumiwa.
Mbinu za maelezo zilitumika katika uwasilishaji wa data.
Mchakato hufanywa kwa kufuata kanuni mahsusi zinazoitwa kanuni geuzi.
Ugeuzi unafuata utaratibu maalum, haufanywi kiholela.
Katika ugeuzi wa maumbo kuna sharti la ukaribu ambapo hakuna kiambajengo kinaweza kuhamishwa zaidi ya fundo funge mbili kutokana na matokeo ya utafiti huu.
Kanuni zingine za uhamisho ni kanuni ya ufungami ambapo muundo wa kijenzi kilichofundwa unahitaji uamuliwe na neno tawala linalofaa.
Kuna vilele kanuni ya ulafi, kanuni teta na kanuni hamishe.
Mwisho kuna kanuni muundo virai, kanuni geuzi na kanuni za mofofonemiki.
Utafiti huu unapendekeza kuwa utafiti zaidi unaweza kufanywa kuhusu aina zingine za mageuzi kama vile, geuzi hamishi swalifu, geuzi hamishi la yambwa tendewa katika lugha hii na hata lugha nyinginezo ili kukuza uwanja wa kisintaksia.
Kuna uhamisho unaotokea kwa lugha zingine na siyo katika Ekegusii.
Hizi pia zinaweza kufanyiwa utafiti.
Tafiti zaidi zinaweza kufanyiwa mada hii kwa kutumia nadharia zingine ili kueleza ikiwa kutakuwa na matokeo tofauti.
Related Results
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Kupambanua Kanuni Zinazotawala Mageuzi katika Sentensi Sahili ya Ekegusii Language in Kenya.
Utafiti huu unalenga kupambanua kanuni zinazotawala mageuzi katika sentensi sahili ya Ekegusii language in Kenya. Nadharia ya Sintaksia Finyizi na Sarufi Geuza Maumbo uliongoza uta...
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.
Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahili ya Ekegusii. Utafiti huu ulihasisiwa na nadharia ya Sintaksia Finyizi. Utafiti...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Uambikaji wa Viambishi Ngeli katika Nomino Sahili Zinazorejelea Ndugu na Maana yake katika Sarufi ya Kiswahili
Nomino sahili ni maneno ambayo kimofolojia yameundwa na mofu huru moja. Pia, kisematiki, maneno haya yana maana zake katika kamusi. Licha ya kuwa na sifa hizi, uambikaji wa viambis...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Jinsi Masuala ya Kijinsia Yalivyo Shughulikiwa Katika Tamthilia ya ‘Bembea ya Maisha’ kwa Kuzingatia Jinsia ya Mwandishi
Maumbile ya binadamu yamechukua mikondo miwili; mwanamume na mwanamke. Jamii tofauti hutoa majukumu kwa kuzingatia migao hii miwili. Hivi ni kusema kuwa, shughuli za mtu katika jam...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Mchango wa Mikakati ya Upole Katika Mazungumzo ya ibada ya Mazishi katika Lugha ya Kikabrasi
Swahili
Suala la upole limetafitiwa na wasomi wengi kwenye mawasiliano, ikiwemo mazungumzo ya abiria na wahudumu wa magari ya uchukuzi kwa lugha ya Kikamba. Hata hivyo, utafiti huu...

