Javascript must be enabled to continue!
Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili
View through CrossRef
Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema (1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu za Jadi, (2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi. Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya. Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002). Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule. Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume. Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya. Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja. Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini.
CARI Journals Limited
Title: Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili
Description:
Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema (1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu za Jadi, (2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi.
Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya.
Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002).
Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume.
Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume.
Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule.
Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani.
Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina.
Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu.
Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume.
Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya.
Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja.
Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini.
Related Results
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Kuchunguza Sababu Zinazowalazimu Wahusika Kufanya Ukahaba katika Riwaya ya Nyota ya Rehema Na Ndoto ya Almasi
Utafiti huu ulichunguza suala la ukahaba katika riwaya ya Nyota ya Rehema (Mohamed S.Mohamed) na Ndoto ya Almasi (Ken Walibora). Kitendo cha ukahaba kimesababisha mashaka mengi san...
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Ukiushi wa Kaida Tagusani katika Kusawiri Upotovu wa Maadili katika Jamii: Mifano kutoka Riwaya Teule za Ken Walibora
Hulka za wahusika katika tungo za sanaa aghalabu husukwa kutokana na matendo yanayoathiriwa na matukio katika mazingira wanamokulia. Hulka hizi hudhihirika kupitia matamko yanayoba...

