Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Usawiri Wa Maradhi Sugu Yanayodhoofisha Mwili Katika Riwaya Teule Za Kiswahili

View through CrossRef
Maradhi ni mojawapo ya matatizo ya kimaumbile yaliyotaabisha binadamu duniani kote kwani asilimia kubwa ya maradhi hayo hayakujulikana vyanzo vyake licha ya utafiti wa kisayansi kuimarika duniani. Binadamu msomi na asiyesoma huishi na wasiwasi kila uchao kwani hajui litakaloathiri mwili wake kesho; hali ambayo hutoa taswira ya maisha kama jinamizi lisilotabirika. Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (2019) unaonyesha kuwa ongezeko la maradhi sugu duniani linatokana na vyakula na vinywaji anavyotumia binadamu vilivyojaa kemikali za kila aina ambazo hutumiwa na mwanadamu katika shughuli za kilimo hususan wakati wa upanzi, ukuzaji, uvunaji na pia uhifadhi wa nafaka. Vilevile, Shirika hili lilibainisha wazi kuwa ongezeko la maradhi husababishwa na mazingira chafu anamoishi mwanadamu na pia mtindo wa maisha katika jamii ya kisasa. Azma kuu ya utafiti ilikuwa kuchunguza usawiri wa maradhi sugu yanayodhoofisha mwili katika riwaya teule. Mtafiti alianuia kuchunguza jinsi mwili wa binadamu uliodhoofishwa na maradhi sugu unavyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili. Malengo mahususi yalikuwa; kudadavua kiini cha ongezeko la maradhi sugu yadhoofishayo mwili wa binadamu kwa mujibu wa riwaya teule, kutathmini athari za maradhi hayo sugu na kisha kuchanganua juhudi za wanajamii kukabiliana na maradhi sugu zinavyosawiriwa katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi. Nadharia hii inatilia mkazo kuwa juhudi za mwanadamu kupambana na maisha huishia katika kukata tamaa pamoja na. Mtafiti aliteua sampuli ya kimaksudi iliyojumuisha riwaya mbili ambazo ni: Kala Tufaha ya Omar Babu na Safari ya Lamu ya John Habwe zilizoandikwa katika karne ya ishirini na moja. Mtafiti alitumia mbinu ya utafiti wa maktaba kudurusu maandishi mbalimbali yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti. Mtafiti alitumia mbinu za kimaelezo ili kuchambua na kuwasilisha data yake akiongozwa na mihimili ya nadharia ya Udhanaishi. Matokeo ya utafiti huu yatachangia pakubwa katika kuhamasisha jamii kuhusu maradhi sugu yanayodhoofisha mwili
Title: Usawiri Wa Maradhi Sugu Yanayodhoofisha Mwili Katika Riwaya Teule Za Kiswahili
Description:
Maradhi ni mojawapo ya matatizo ya kimaumbile yaliyotaabisha binadamu duniani kote kwani asilimia kubwa ya maradhi hayo hayakujulikana vyanzo vyake licha ya utafiti wa kisayansi kuimarika duniani.
Binadamu msomi na asiyesoma huishi na wasiwasi kila uchao kwani hajui litakaloathiri mwili wake kesho; hali ambayo hutoa taswira ya maisha kama jinamizi lisilotabirika.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (2019) unaonyesha kuwa ongezeko la maradhi sugu duniani linatokana na vyakula na vinywaji anavyotumia binadamu vilivyojaa kemikali za kila aina ambazo hutumiwa na mwanadamu katika shughuli za kilimo hususan wakati wa upanzi, ukuzaji, uvunaji na pia uhifadhi wa nafaka.
Vilevile, Shirika hili lilibainisha wazi kuwa ongezeko la maradhi husababishwa na mazingira chafu anamoishi mwanadamu na pia mtindo wa maisha katika jamii ya kisasa.
Azma kuu ya utafiti ilikuwa kuchunguza usawiri wa maradhi sugu yanayodhoofisha mwili katika riwaya teule.
Mtafiti alianuia kuchunguza jinsi mwili wa binadamu uliodhoofishwa na maradhi sugu unavyosawiriwa katika riwaya teule za Kiswahili.
Malengo mahususi yalikuwa; kudadavua kiini cha ongezeko la maradhi sugu yadhoofishayo mwili wa binadamu kwa mujibu wa riwaya teule, kutathmini athari za maradhi hayo sugu na kisha kuchanganua juhudi za wanajamii kukabiliana na maradhi sugu zinavyosawiriwa katika riwaya teule.
Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi.
Nadharia hii inatilia mkazo kuwa juhudi za mwanadamu kupambana na maisha huishia katika kukata tamaa pamoja na.
Mtafiti aliteua sampuli ya kimaksudi iliyojumuisha riwaya mbili ambazo ni: Kala Tufaha ya Omar Babu na Safari ya Lamu ya John Habwe zilizoandikwa katika karne ya ishirini na moja.
Mtafiti alitumia mbinu ya utafiti wa maktaba kudurusu maandishi mbalimbali yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti.
Mtafiti alitumia mbinu za kimaelezo ili kuchambua na kuwasilisha data yake akiongozwa na mihimili ya nadharia ya Udhanaishi.
Matokeo ya utafiti huu yatachangia pakubwa katika kuhamasisha jamii kuhusu maradhi sugu yanayodhoofisha mwili.

Related Results

Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Mtagusano wa Vipengele vya Utandawazi na Vipengele vya Falsafa ya Ubuntu katika Riwaya Teule za Kisasa za Kiswahili
Riwaya za kisasa ni zile zilizoandikwa katika zama za utandawazi na huakisi maisha, changamoto, na mitazamo ya dunia ya sasa. Tofauti na riwaya zisizo za kisasa au za mwanzo zinazo...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Uchunguzi Linganishi wa Dhamira Zinazowasilishwa Kupitia Wahusika wa Kiume Katika Riwaya Teule za Kiswahili
Makala hii inalinganisha dhamira zilizowasilishwa kupitia wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake wa Kenya na Tanzania. Tumaini (2006) ya Clara...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Uundaji wa Kauli ya Kutendwa Katika Lugha ya Kiswahili na ya Kiarabu
Utafiti huu unalenga kuchanganua na kuchunguza uundaji wa kauli ya kutendwa katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiarabu, na mtafiti kutokana na ufundishaji wake wa kozi za sarufi...

Back to Top