Javascript must be enabled to continue!
Tamthilia ya Kiswahili katika Ukuaji na Ustawi Endelevu wa Ujasiriamali Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari
View through CrossRef
Ujasiriamali ni wimbo unaozidi kurindima masikioni mwa wanajamii. Wimbo huu unatokana na changamoto ya fursa funge za ajira miongoni mwa vijana. Tatizo linaonekana kuwa kubwa kwa sababu vijana wengi hawaonekani kuwa na msukumo wa ndani na wa kimazingira wa kujiajiri. Vijana wengi bado wanaamini katika kuajiriwa badala ya kujiajiri ilhali fursa za ajira rasmi wazitakazo ni chache kuliko idadi yao. Serikali na wadau wa maendeleo, wanazidi kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii ya ajira miongoni mwa vijana. Mojawapo ya mapendekezo ya kutatua changamoto hii, ni kwa serikali na wadau kuwawezesha vijana kujikomboa kifikra kupitia elimu na mazingira rafiki kwa ujasiriamali. Baadhi ya wadau, wanaamini elimu rasmi ya ujasiriamali katika shule ya msingi na sekondari ndiyo suluhu kwa vijana kufikiria kujiajiri. Hata hivyo, kuna hoja kuwa wadau wa elimu wamechelewa sana kuiteua tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari kuwa tamthilia ya kiada miongoni mwa tamthilia rasmi zinazopaswa kufundishia na kujifunza uhakiki wa fasihi na ujasiriamali katika ngazi ya sekondari na vyuo. Hivyo, makala haya yanawasilisha sehemu ya matokeo ya uchunguzi tulioufanya kuhusiana na maudhui ya tamthilia ya Safari ya Chinga ili kuonesha nafasi adhimu ya Tamthilia ya Kiswahili katika ukuaji na ustawi endelevu wa ujasiriamali nchini Tanzania.
East African Nature and Science Organization
Title: Tamthilia ya Kiswahili katika Ukuaji na Ustawi Endelevu wa Ujasiriamali Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari
Description:
Ujasiriamali ni wimbo unaozidi kurindima masikioni mwa wanajamii.
Wimbo huu unatokana na changamoto ya fursa funge za ajira miongoni mwa vijana.
Tatizo linaonekana kuwa kubwa kwa sababu vijana wengi hawaonekani kuwa na msukumo wa ndani na wa kimazingira wa kujiajiri.
Vijana wengi bado wanaamini katika kuajiriwa badala ya kujiajiri ilhali fursa za ajira rasmi wazitakazo ni chache kuliko idadi yao.
Serikali na wadau wa maendeleo, wanazidi kukuna vichwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto hii ya ajira miongoni mwa vijana.
Mojawapo ya mapendekezo ya kutatua changamoto hii, ni kwa serikali na wadau kuwawezesha vijana kujikomboa kifikra kupitia elimu na mazingira rafiki kwa ujasiriamali.
Baadhi ya wadau, wanaamini elimu rasmi ya ujasiriamali katika shule ya msingi na sekondari ndiyo suluhu kwa vijana kufikiria kujiajiri.
Hata hivyo, kuna hoja kuwa wadau wa elimu wamechelewa sana kuiteua tamthilia ya Safari ya Chinga (2009) ya Shani Omari kuwa tamthilia ya kiada miongoni mwa tamthilia rasmi zinazopaswa kufundishia na kujifunza uhakiki wa fasihi na ujasiriamali katika ngazi ya sekondari na vyuo.
Hivyo, makala haya yanawasilisha sehemu ya matokeo ya uchunguzi tulioufanya kuhusiana na maudhui ya tamthilia ya Safari ya Chinga ili kuonesha nafasi adhimu ya Tamthilia ya Kiswahili katika ukuaji na ustawi endelevu wa ujasiriamali nchini Tanzania.
Related Results
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili
Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha matukio ya fasihi andishi na jinsi yanavyoichora na kwa mapana kuwa kioo cha jami...
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Visababishi vya Idadi Kubwa ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Uganda Kutochukua Somo la Kiswahili
Katika makala haya, mtafiti anaeleza visababishi vya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za upili nchini Uganda kutochukua somo la Kiswahili. Wakati wa kupunguza idadi ya masomo ...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia
Purpose
Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidiji...
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Athari ya Ukosefu wa Ishara za Isimu katika Ufundishaji na Athari ya Mikato ya Kiingereza na Kiswahili katika Uchapishaji wa Vitabu
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usimilishaji wa ishara za isimu katika breili ya Kiswahili. Uchanganuzi huu ulitiwa hamasa na mambo matano muhimu. Kwanza, breili ndio njia ya pekee...
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Maisha ya Penina Muhando na Mchango wake katika Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili
Penina Muhando ni mwanazuoni aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya fasihi na lugha ya Kiswahili. Mchango wake umeonekana hasa katika tamthiliya, sanaa za maonyesho pamoja na ...
Vikwazo vya Usimilishaji wa Ishara za Isimu katika Breili