Search engine for discovering works of Art, research articles, and books related to Art and Culture
ShareThis
Javascript must be enabled to continue!

Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014

View through CrossRef
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia. Mbinu iliyotumika ni ya maktabani ambapo mwandishi alisoma na kuhakiki maudhui ya SEM msisitizo ukiwa kwenye masuala yahusuyo lugha ya kufundishia. Uchambuzi wa kiisimujamii ulitumika ili kuonesha ukinzani baina ya matamko ya SEM. Tamko la SEM kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia haliakisi hali halisi. Uhusiano wa Kiisimujamii wa lugha ya Kiswahili na ya Kiingereza kuhusu elimu unatoa tafsiri kuwa endapo SEM itatumika bila nia ya dhati ya kuisaidia lugha ya Kiswahili basi lugha hiyo inaweza kutoweka kabisa kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia. Makala yanajenga hoja kuwa tamko la SEM kwamba Kiingereza na Kiswahili ziwe na hadhi sawa kwenye mfumo wa elimu linatia moyo kwa mustakabali wa lugha ya Kiswahili lakini utekelezaji wake unaibua changamoto nyingi kwa namna ambayo zisipotazamwa kwa makini lugha ya Kiingereza itaendelea kukita mizizi zaidi na kujenga uwezekano wa jamii kukataa kufundishwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu mwelekeo wa jamii unanasibisha elimu na Kiingereza. Mwisho, wito unatolewa kwa watunga sera kusitisha kutumia lugha ya wachache kutoa elimu kwa wengi kwa kuwa kufanya hivyo ni kubadili malengo ya elimu.
Mkwawa University College of Education
Title: Mustakabali wa Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia Nchini Tanzania: Uhakiki wa Maudhui ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014
Description:
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014).
Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia.
Mbinu iliyotumika ni ya maktabani ambapo mwandishi alisoma na kuhakiki maudhui ya SEM msisitizo ukiwa kwenye masuala yahusuyo lugha ya kufundishia.
Uchambuzi wa kiisimujamii ulitumika ili kuonesha ukinzani baina ya matamko ya SEM.
Tamko la SEM kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia haliakisi hali halisi.
Uhusiano wa Kiisimujamii wa lugha ya Kiswahili na ya Kiingereza kuhusu elimu unatoa tafsiri kuwa endapo SEM itatumika bila nia ya dhati ya kuisaidia lugha ya Kiswahili basi lugha hiyo inaweza kutoweka kabisa kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia.
Makala yanajenga hoja kuwa tamko la SEM kwamba Kiingereza na Kiswahili ziwe na hadhi sawa kwenye mfumo wa elimu linatia moyo kwa mustakabali wa lugha ya Kiswahili lakini utekelezaji wake unaibua changamoto nyingi kwa namna ambayo zisipotazamwa kwa makini lugha ya Kiingereza itaendelea kukita mizizi zaidi na kujenga uwezekano wa jamii kukataa kufundishwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu mwelekeo wa jamii unanasibisha elimu na Kiingereza.
Mwisho, wito unatolewa kwa watunga sera kusitisha kutumia lugha ya wachache kutoa elimu kwa wengi kwa kuwa kufanya hivyo ni kubadili malengo ya elimu.

Related Results

Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Mabadiliko katika Mtaala wa Elimu ya Msingi na Namna Yanavyoathiri Tathmini katika Elimu ya Juu
Makala haya yamekusudia kuchunguza namna ambavyo mabadiliko katika mtaala wa elimu ya msingi yanavyoathiri tathmini katika elimu ya juu. Mabadiliko ya mtaala yanafanyika katika nga...
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Ushairi WA Kiganda Unavyoweza Kuchangia Na Kuendeleza Ushairi WA Kiswahili Kimtindo Na Kimaudhui: Mfano WA Ufundishaji Nchini Uganda
Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugumu katika kujifunza ushairi wa Kiswahili. Ushairi wa Kiganda umekuwa unatendwa v...
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Mikakati ya Urekebu wa Kiswahili kama Lugha Rasmi Nchini Kenya
Makala haya yanajadili jinsi Kiswahili kilivyokubalika kama lugha rasmi nchini Kenya baada ya kuidhinishwa kwa Katiba ya 2010, na maswali yaliyoibuka kuhusu uwezo wake katika mawas...
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Matumizi ya Lugha Kwenye Malezi ya Watoto: Mfano wa Matumizi ya Semi Katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli yao ya kulea watoto. Alifanya hivyo kwa kurejelea malezi ya watoto katika jamii ya Wamasaaba...
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Athari ya Mitindo Mbalimbali ya Breili katika Unukuzi wa Maandishi ya Breili ya Kiswahili
Utafiti huu ulinuia kuchanganua usahihi wa unukuzi wa maandishi ya breili hadi maandishi ya kawaida na kinyume chake, ili kuleta maana iliyokusudiwa. Katika kutimiza lengo hilo, ut...
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Mapokezi ya Nomino za Kiswahili katika Ngeli za Nomino za Gᴉrᴉmi
Ikisiri Lengo la makala hii ni kuonesha jinsi nomino za Kiswahili zinavyokopwa ili kukidhi mawasiliano katika Gᴉrᴉmi. Nomino (majina) ni miongoni mwa maneno yanayokopwa kutokana na...
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Matumizi ya Lugha katika Tamthiliya ya ( Sadaka ya John Okello )
Kipengele hiki hakipatikani katika lugha zote (bonyeza chache tu). Grafu iliyotangulia Ni ngapi huduma hii haipatikani katika lugha zote. Chini ni orodha ya kurasa zetu maarufu za ...
The Englishization of Tanzanian Kiswahili
The Englishization of Tanzanian Kiswahili
ABSTRACT: The paper discusses the influence of English on Kiswahili, namely, the Englishization of Kiswahili on the basis of data extracted from various recent textbooks, pop stor...

Back to Top